Ummu Aliy

VIPIMO
Kara-biskuti tamu 450 gms au 16 oz
(Puffy Crispy Biskuits)
au
(Biscuits Feuilletés)
Maziwa Lita (litre) 1 na 1/4
Malai (cream) 340 gms au 12 oz
Samli 3 vijiko vya supu
Sukari 1/2 kikombe au zaidi
Njugu za Pistachio
(zilizokatwa ndogo ndogo) 1/2 Kikombe
Lozi (zilizokatwa ndogo ndogo) 1/2 kikombe
Zabibu kavu 1/2 kikombe
Vanilla 1 kijiko cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Katakata kara-biskuti
2. Chemsha maziwa pamoja na samli, sukari, njugu za pistachio, lozi, zabibu.
3. Tia vanilla koroga ichanganyike vizuri.
4. Ikichemka epua na mwagia kwenye kara-biskuti.
5. Tupia malai (Cream) juu yake ieneze vizuri.
6. Pika katika moto wa 400º kwa muda wa dakika 20 au hadi ikauke na kara-biskuti zigeuke rangi kidogo kwa juu.
7. Tayari kuliwa.
VIDOKEZO:
1. Inaweza kuliwa ikiwa ya vuguvugu na sio lazima iwe baridi.
2. Unaweza kutumia mikate yake khaswa ya kupikia Ummu 'Aliy inayouzwa katika bekari au tumia puff-pastry, uipikie kwanza katika oveni hadi iwive kisha ichambue chambue
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


