Kufanya Kazi Katika Duka Au Sehemu Inayouzwa Nyama Ya Nguruwe

  SWALI LA KWANZA:

 

assalam allaikum warahmatullahi wabarakat?kwanza kabisa,ningependa kuwashukuru sana kwa kutuelimisha kwa mambo mengi..Mola awape ajar zake inshAllaah....nina swali moja inshAllaah

mimi ninafanya kazi katika duka moja hapa ulaya ambalo lina sehemu nyingi...mara kadha niko sehemu tofauti.Sehemu zenyewe ni,sehemu ya maziwa,nyama na madawa...katika sehemu ya nyama huwa wanatayarisha nyama kadha ya ng'uruwe ikiwemo...nimemweleza meneja kama ni haramu kwa mwislamu kutayarisha chochote chenye ng'uruwe.ameniahidi atanitoa hiyo sehemu lakini hadi sasa hajatia bidii kunibadilisha....nina wasiwasi kila siku ingawa niko hiyo sehemu siku moja kila wiki....nifanye nini?

shukran.

wabilahi tawfiq.....

  

SWALI LA PILI:

 

asalam alaikum w w ndugu zangu ktk uislam kwanza nina towa shukurani zangu za dhati kwa uhodari na ufasaha wenu ktk kutusaidia sisi ambao hatuku bahati kujuwa kitabu cha mwenyezi mungu na sunna za kiongozi wa umma wetu wa kiislam ok kwa kweli ndugu nina shukuru pia nakutakieni kila kheiri kwa muumba hapa duniani na huko mbele ya haki

 

 

ok NB ndugu zangu masheikh wangu mimi swali langu ni hili JE MUISLAM ANA RUHUSIWA KUFANYA KAZI YA KU FAGIA SEHEMU AMBAPO KUNA SINDIKWA NYAMA YA NGURUWE? KTK KIWANDA CHA AINA YOYOTE ILE KINACHO SHUHULUKIA VITU AMBAVYO VINA TOKANA NA NGURUWE? eh ndugu zangu kama jinsi nilivyo jitambulsha hapo mwanzoni mimi ni kijana wa kiislam nina ishi ulaya yani ktk nchi ya nederland sasa nimepata kazi sehemu hiyo je nina ruhuwa kidini kiifanya au, naomba ufafanu kwa kina kwa sababu yuko kijan mmoja ambaye ni rafiki yangu yeye ni muislam na anafanya kazi huko sasa yeye aliniambiya kuwa ali uliza wana chuoni wa huko kwao yani yeye ni mtu kutoka africa magharibi wakamuambia eti ina juzu isipokuwa labda yeye kuchinja ndio kharam sasa nakuombeni msi ni puuzie ili nipate jibu haraka nisije nika tumbukia , kwa hiyo nakutakieni usikivu mwema wa billaihi tawfiq……….

 

ma sheikh zangu nilikuwa nime sahau kidogo yani sehemu ile sio sehemu wanayo chinjia nguruwe ila ni sehemu ambayo yama hiyo ina tengenezwa na kupakia ktkt mifuko maalum na mimi kizili omba niya kufanya usafi kam vile kusafisha sakafu na meza na sehemu nyingine pia nimeambiwa kuwa vipo vifaa maalum una tumia kama glovs na..... ok yani jamaa yangu kaniambia kuwa eti mtu huwa hugusi hiyo nyama wabillaihi tawfiq

 

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola  wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Kufanya kazi yoyote inayohusiana na yale yaliyoharamishwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) ikiwa ni nguruwe, pombe, kamari n.k. inapasa kuepukana nayo kwa kila njia. Katika hali ya waulizaji ambayo ni nguruwe, kazi iwe ya kuchinja nguruwe, kusafisha sehemu wanazofugwa, kupakia nyama katika paketi, kuuza nyama au vitu vyovyote vinavyohusiana nayo basi huwa ni haraam. Hii ni sawa sawa na kulingana na hali katika kauli ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa alihi wa sallam) ifautayo inayohusiana na pombe:   

عن أنس قال  : لعن رسول الله صلى الله عليه وسلم في الخمر عشرة : عاصرها , ومعتصرها , وشاربها , وحاملها , والمحمولة إليه , وساقيها , وبائعها , وآكل ثمنها , والمشتري لها , والمشتراة له   رواه الترمذي وابن ماجه

Kutoka kwa Anas kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amelaani mambo kumi yanayohusiana na ulevi; mwenye kuukamua (kuutengeneza), Mwenye kutengenezewa, mnywaji, mbebaji, anayebebewa, anayeendesha (kuupeleka ulevi), muuzaji, anayekula thamani yake, anayenunua na anayeuza. [At-Tirmidhiy na Ibn Maajah)

Maelezo zaidi ya makatazo ya kazi hizo, yanapatikana katika kiungo kifutacho chenye Swali kama hilo: 

Ninafanya Kazi Ya Kuchinja Nguruwe, Je, Halali? 

Tunawapa nasaha wote baada ya kupata maelezo marefu yanayohusu uharamu wa kufanya kazi ya aina yoyote inayohusiana na yaliyoharamishwa kama nguruwe au pombe n.k. kuwa mcheni Allaah, na muache yaliyoharamishwa na mtafute kazi sehemu nyingine isiyochanganya yaliyo haramu. Naye Allaah Ndiye Mwenye Kuwaruzuku. Na mtakapomtegemea Atakufungulieni milango ya kheri mingi kama Anavyosema:

(( وَمَن يَتَّقِ اللَّهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا))  

((Na anayemcha Allaah Humtengezea njia ya kutokea)) [At-Twalaaq: 2]

(( وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لاَ يَحْتَسِبُ وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ فَهُوَ حَسْبُهُ إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ  لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْرًا))

((Na Humruzuku kwa njia asiyotazamia. Na anayemtegemea Allaah Yeye Humtosha. Hakika Allaah Anatimiza amri Yake. Allaah  Kajaalia kila kitu na kipimo chake))   [At-Twalaaq: 3]

(( وَمَن يَتَّقِ اللَّهَ يَجْعَل لَّهُ مِنْ أَمْرِهِ يُسْرًا ))

((Na anayemcha Allaah, Humfanyia mambo yake kuwa mepesi)) [At-Twalaaq: 4]

Vile vile mwenye kuacha jambo kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atamruzuku lililo bora na la kheri kuliko hilo alivyosema Mtume wetu Mkweli Mwaminifu:

 

  ((إنك لا تدع شيئاً إتقاء لله تعالى إلا أعطاك الله عز وجل خيراً منه))   رواه أحمد والبيهقي وهو حديث صحيح

 

((Huachi jambo kwa ajili ya kumcha Allaah Ila Atakupa Allaah 'Azza wa Jalla lililo na kheri kuliko hilo)) [Ahmad, Al-Bayhaqiy nayo ni Hadiyth Swahiyh] 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 


Share