Pilau Ya Tuna Na Mboga

Vipimo
Mchele 2 Mugs
Mboga mchanganyiko za barafu 1 Mug
(Frozen veg)
Tuna 2 kopo
Thom na tangawizi 2 vijiko vya supu
Garam masala 1 kijiko cha supu
Nyanya 2
Kitungu maji 1
Mdalasini nzima 2 vijiti
Karafuu 6 chembe
Pilipili mbichi 1
Chumvi kiasi
Viazi 3
Maji 2 ½ Mugs
Mafuta 3 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha mchele na uroweke kwa muda wa dakika 20
- Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji mpaka kigeuke rangi ya hudhurungi (brown).
- Mimina viazi, thomu na tangawizi, bizari zote na kaanga.
- Tia nyanya uliyokatakata ikaange mpaka iwive.
- Tia tuna endelea kukaanga kidogo tu.
- Tia maji, yatakapochemka tia mchele.
- Punguza moto uwe mdogo funika kwa muda wa ½ saa hadi wali ukauke na uwive. Utakuwa tayari kuliwa.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha

Asalaam alykhum, sina mengi
Asalaam alykhum, sina mengi isipokuwa ni shukrani tu nyingi kwa kutuelimisha kwa mafundisho mbalimbali ya elmu ya dini na dunia.Ama kwa hakika nimejifunza mengi hasa kipindi cha mwezi mtukufu wa ramdhani.Namuomba ALLAH azidi kuwatia nguvu na moyo na imani mzidi kutuelimisha.
Inshaalahu.