Sababu Za Kuwa Na Miezi Mitukufu

SWALI:

 

 

nilikuwa na masuala yafuatayo.

 

katika kuran tukufu suratul tawbah aya 35 kumetajwa kuhusu miezi mitukufu nayo ni 4,dhul qaidah(huu uloanza leo),dhul hijjah,muharam na rajab. sualalangu,nataka kujua    a)jee kuna kisa gani kulitokea mpaka ikawa mitukufu hiyo miezi.b) kuna ibada za sunna za kufunga ktk miezi hii,jee zikoje duas za kuomba n.k

shukrani sana.

 


 

 

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Kuhusu ibada za kutekeleza katika miezo mitukufu hii tayari tumeshakujibu kwa kukutumia makala inayoelezea yote yapasayo kufanya na kujiepusha nayo ambayo inapatikana katika kiungo kifautacho:

 

 

Tumeingia Katika Miezi Mitukufu Inatupasa Kuitakasa Kwa Kuacha Maovu Na Kuzidisha Mema

 

 

Miezi mitukufu hiyo ambayo imetajwa katika usimulizi ufuatao ilijulikana kuwa ni mitukufu tokea zama za ujaahiliyyah (Kabla ya Uislamu):

 

 

عَنْ أَبَى بَكْرَة أَنَّ رَسُول اللَّه - صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ - قَالَ فِي حَجَّة الْوَدَاع : ((إِنَّ الزَّمَان قَدْ اِسْتَدَارَ كَهَيْئَتِهِ يَوْم خَلَقَ اللَّه السَّمَوَات وَالْأَرْض السَّنَة اِثْنَا عَشَر شَهْرًا مِنْهَا أَرْبَعَة حُرُم : ثَلَاث مُتَوَالِيَات ذُو الْقَعْدَة وَذُو الْحِجَّة وَالْمُحَرَّم وَرَجَب مُضَر الَّذِي بَيْن جُمَادَى وَشَعْبَان))  صَحِيح الْبُخَارِيّ

Kutoka kwa Abu Bakrah ambaye amesema: 'Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema alipokuwa katika Hijjah ya kuaga (Hijjah yake ya mwisho kabla ya kufa): ((Mgawanyo wa nyakati umerudi kama ulivyo (wakati) Allaah Alipoumba mbingu na ardhi. Mwaka una miezi kumi na mbili, minne ambayo ni mitukufu; mitatu inafuatana pamoja (nayo ni) Dhul-Qa'adah, Dhul-Hijjah na Muharram, na (wa nne ni) Rajab wa (kabila la) Mudhwar ambao upo baina ya Jumaada na Sha'abaan)) [Al-Bukhaariy)

 

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameelezea zaidi kwamba ‘Rajab ya Mudhwar’ ni kwa ajili ya kuthibitisha kauli ya Mudhwar wanayosema kwamba Rajab ni mwezi baina ya Jumaadah na Sha’baan na sio kama walivyodhani kabila la Rabiy’ah kwamba uko baina ya Sha’baan na Shawwaal ambao ni Ramadhaan katika kalenda ya sasa.

 

Miezi minne hiyo ambayo mitatu inafuatana na mmoja uko pekee ili iwezekane kutekelezwa ibada ya Hajj na ‘Umrah kwa wepesi.

 

Dhul-Qa’adah: mwezi wa kabla ya Hajj umefanywa mtukufu kwa sababu walijizuia kupigana katika mwezi huo.

 

Dhul-Hijjah: umefanywa mtukufu kwa sababu ni mwezi wa Hjja ambao taratibu za Hajj zinatekelezwa (na kukamilishwa) humo.

 

Muharram: unaofuatia, umefanywa mtukufu ili watu waweze kurudi makwao kwa usalama (baada ya kutekeleza Hajj).

 

Rajab: ambao ni katikati ya mwaka, umefanywa mtukufu ili watu waliokuwa wanakuja kutoka pande za mbali za bara la Arabuni waweze kufanya ‘Umrah na kutembelea Nyumba (Ka’bah) kisha warudi makwao kwa usalama.  [Tafsiyr Ibni Kathiyr]

 

Hayo ndiyo tuliyoweza kuyapata katika maelezo ya miezi mitukufu hiyo na sababu zake.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share