Hii Ndiyo Itikadi Sahihi Ya Kiislamu
Sheikh Muhammad Bin 'Uthaymiyn
Imetarjamiwa Na Muhammad Faraj
Shukrani zote ni zake Mola wa uliwengu wote, na mwisho mwema ni wa wamchao Mwenyezi Mungu, na hapana uadui isipokuwa kwa madhalimu.
Nashuhudia kuwa hapana anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allaah Peke yake asiye na mshirika mwenye Ufalme na haki iliyo wazi, na nashuhudia kuwa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni mjumbe wake na Mtume wake na mwisho wa wajumbe wake, na ni kiongozi wa wacha Mungu. Mola wetu msalie na msalimie Mtume wako huyu pamoja na Masahaba wake na kila atakayemfuata kwa wema na uongofu mpaka Siku ya Kiama.
Amma baad,
Hakika Mwenyezi Mungu amemtuma Mtume wake Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) awe dalili iliyo wazi juu ya waja wake wote, na awabainishie yale aliyoteremshiwa katika kitabu, na awe mfano mwema wa kuigwa na walimwengu wote, na ili watu wapate kuwa na muongozo mwema katika dini
Ametumwa kutufundisha itikadi sahihi pamoja na hekima kwa ajili ya kutengenea hali za umma wake na kuwaweka juu ya njia safi na sahihi, ili watu wawe juu ya kitanga cheupe, mchana wake sawa na usiku wake, na asende kinyume na njia hiyo isipokuwa mpotofu.
Wakaifuata njia hiyo Masahaba wake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na wale waliokuja baada yao na waliowafuatilia kwa wema, wakaisimamisha sheria ya Mwenyezi Mungu na kuyakamata mafundisho hayo kwa magego yao kwa kuifuata itikadi hii iliyo sahihi, na ibada na mwenendo na tabia. Na sisi Alhamdulillah tunaendelea kuufuata mwenendo wao huo kwa kufuata dalili zilizomo ndani ya Qurani na zilizomo ndani ya mafundisho yake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na tunamuomba Mwenyezi Mungu atuthibitishe juu ya njia hiyo sisi na ndugu zetu wote wa Kiislamu kwa kauli iliyo thabit katika maisha ya duniani na ya akhera na atumiminie rehma Zake kwani yeye ni Mwenye kutoa kwa wingi.
Kutokana na umuhimu wa maudhui haya, na kutokana na tofauti iliyokuja baadaye, baada ya kuingizwa matamanio ya watu ndani ya itikadi hii, nilipenda kuiandika iwe kama ndiyo itikadi yetu, Itikadi ya Ahli Sunnah wal Jama-a, nayo ni imani ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu na Malaika wake na vitabu vyake na Mitume yake na Siku ya Kiama na Qadar (qudra) kheri yake na shari yake.
Namuomba Mwenyezi Mungu aijaalie kazi hii iwe halisi kwa ajili yake, Aridhike nayo na iwe funzo kwa waja Wake.
Itikadi yetu;
Itikadi yetu ni kumuamini Mwenyezi Mungu na Malaika Wake na Mitume Yake na Vitabu Vyake na Siku ya Mwisho na Qadar kheri yake na shari yake (kuwa inatoka kwa Mwenyezi Mungu).
Kwa hivyo sisi tunaamini kuwa Yeye Subhanahu wa Taala ndiye aliyeumba na ndiye Mfalme Mwenye kukiendesha kila kitu, na ni Yeye peke yake anayestahiki kuabudiwa, na kila kinachoabudiwa kisichokuwa Yeye ni batil.
Tunaamini pia kuwa Mwenyezi Mungu ana majina mazuri mazuri na sifa nzuri nzuri na njema, sifa za ukamilifu, na tunaamini kuwa Yeye ni mmoja asiye mshirika katika kuumba Kwake na katika kuabudiwa Kwake na katika majina Yake mazuri na katika sifa Zake njema.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake. Basi muabudu Yeye tu, na udumu katika ibada yake. Je, mnamjua mwenye jina
Maryam – 65
Na tunaamini kuwa Yeye ndiye;
"Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye, Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu."
Al Baqarah – 255
Na tunaamini kuwa;
"Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji, Mtia sura, Mwenye majina mazuri kabisa. Kila kilioko katika mbingu na ardhi kinamtakasa, naye ni Mwenye kushinda, Mwenye hikima."
Al Hashr - 22
Na tunaamini kuwa;
"Ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu; anaumba apendavyo, anamtunukia amtakaye watoto wa kike, na anamtunukia amtakaye watoto wa kiume.
Au huwachanganya wanaume na wanawake, na akamfanya amtakaye tasa. Hakika Yeye ni Mjuzi Mwenye uweza."
Al Shuura – 49-50
Na tunaamini kuwa;
"Yeye ndiye Muumba mbingu na ardhi, amekujaalieni mke na mume katika nafsi zenu, na katika wanyama nao (akawaumba) dume na jike, anakuzidishieni namna hii. Hapana kitu
Yeye ndiye Mwenye funguo za mbingu na ardhi. Humkunjulia riziki amtakaye, na humpimia amtakaye. Hakika Yeye ni Mjuzi wa kila kitu."
Ash Shuura – 11-12
Na tunaamini kuwa;
"NA HAKUNA mnyama yoyote katika ardhi ila riziki yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Naye anajua makao yake na mapitio yake. Yote yamo katika Kitabu chenye kubainisha."
Hud - 6
Na tunaamini kuwa;
"Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Yeye anajua kilioko nchi kavu na baharini. Na halidondoki jani ila analijua. Wala punje katika giza la ardhi, wala kinyevu, wala kikavu ila kimo katika Kitabu kinacho bainisha."
Al An Aam – 59
Na tunaamini kuwa;
"Hakika kuijua Saa (ya Kiyama) kuko kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye ndiye anaye iteremsha mvua. Na anavijua viliomo ndani ya matumbo ya uzazi. Na haijui nafsi yoyote itachuma nini kesho. Wala nafsi yoyote haijui itafia nchi gani. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua, Mwenye khabari".
Luqman – 34
Sifa ya kusema;
Tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu anasema wakati wowote anapotaka na kwa njia yoyote anayotaka;
Mwenyezi Mungu anasema;
"Na Mwenyezi Mungu akamsemeza Musa."
An Nisaa – 164
Na akasema;
"Na alipo kuja Musa kwenye miadi yetu, na Mola wake Mlezi akamsemeza."
Al Aaraf – 143
Na akasema;
"Na tulimwita upande wa kulia wa mlima na tukamsogeza kunong'ona naye."
Maryam – 52
Na tunaamini kuwa;
"Lau kama bahari ndio wino kwa maneno ya Mola wangu Mlezi, basi bahari ingeli malizika kabla ya kumalizika maneno ya Mola wangu Mlezi, hata tungeli ileta mfano wa hiyo kuongezea."
Al Kahf – 109
Na timaamini kuwa;
"Na lau kuwa miti yote iliyomo duniani ikawa ni kalamu, na bahari (ikawa wino), na ikaongezewa juu yake bahari nyengine saba, maneno ya Mwenyezi Mungu yasingeli kwisha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima."
Luqman – 27
Na tunaamini kuwa maneno yake ni ya ukamilifu uliokamilika na ya ukweli uliokamilika na yenye uadilifu uliokamilika.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Yametimia maneno ya Mola Mlezi wako kwa kweli na uadilifu. Hapana awezaye kuyabadilisha maneno yake. Na Yeye ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua."
Al An Am - 115
Na akasema;
" Na ni nani msema kweli kuliko Mwenyezi Mungu?"
An Nisaa – 87
Na tunaamini kuwa Qurani ni maneno ya Mwenyezi Mungu, aliyeyatamka kwa uhakika kabisa kwa kumfundisha Jibril aliyeiteremsha mpaka ndani ya kifua cha Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam);
Mwenyezi Mungu anasema;
"Sema: Ameiteremsha hii (qurani) Roho takatifu kutokana na Mola wako Mlezi kwa haki."
An Nahl – 102
Na akasema;
"Na bila ya shaka hii ni Uteremsho wa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Ameuteremsha Roho muaminifu, Juu ya moyo wako, ili uwe katika Waonyaji. Kwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi."
Al Shuaraa – 192 – 195
Kuwepo Kwake Juu 'Al Uluw';
Tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu yupo juu kabisa mbali na viumbe vyake kwa dhati Yake na kwa sifa Zake, na hii inatokana na kauli Yake Subhanahu wa Taala aliposema;
"Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu."
Al Baqarah – 255
(Na akasema;)
("Malaika na roho hupanda kwake katika siku ambayo muda wake ni miaka elfu hamsini.")
Maarij – 4
(Na akasema;)
("Je! Mnadhani muko salama kwa (Mwenyezi Mungu) ambaye yuko mbinguni ya kuwa Yeye hatokudidimizeni ardini tahamaki hiyo inataharaki?")
Al Mulk - 16
Na akasema;
"Naye ndiye Mwenye nguvu juu ya waja wake."
Al An Am -18
(Na katika Sunnah- Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema;
"Mrehemu aliye ardhini atakurehemu aliye mbinguni."
Abu Yaal na Al Tabarani na Al Hakim
Na kuwepo mbinguni hakuna maana kuwa yupo katika mojawapo ya sayari zilizopo juu kama baadhi ya watu wanavyoweza kudhania, bali dunia yetu ukiilinganisha na mbingu ni mfano wa doa doogo sana, bali hata haionekani. Kwani huko juu kuna nyota na sayari zilizoenea hata
Na tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu anayo Arshi Yake
Mwenyezi Mungu anasema;
"Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenyezi Mungu, ambaye ameziumba mbingu na ardhi kwa siku sita, kisha akatawala juu ya Arshi Yake."
Yunus – 3
Na kutawala juu ya Arshi Yake ni kutawala kunakonasibiana na utukufu wake Subhanahu wa Taala, hapana anayejuwa mfano wake isipokuwa Yeye.
Na tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu akiwa juu ya Arshi Yake, yupo pamoja na viumbe vyake kwa elimu yake, anasikia kauli zao na kuona vitendo vyao, huku akiyaendesha mambo
Na Yeyote mwenye uwezo huo, basi bila shaka yupo pamoja na viumbe vyake kikweli huku akiwa juu ya Arshi yake kikweli, na ni Yeye Peke yake ndiye mwenye kuujuwa uhakika wake.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Hapana kitu
Al Shuura – 11
(Mwenyezi Mungu anasema;
"Na Malaika watakuwa kandoni mwake (hizo mbingu) na Malaika wa namna nane watachukuwa Kiti cha enzi cha Mola wako (Arshi) juu
Al Haqqah – 17)
Sisi hatusema kama wanavyosema Al Jahamiyah kuwa eti Mwenyezi Mungu yupo ardhini pamoja na viumbe vyake, na tunaona kuwa kusema hivyo ni kukufuru au ni upotofu, kwa sababu kumpa Mwenyezi Mungu wasfu usiolingana naye ni kupunguza katika sifa Zake.
Kushuka;
Tunaamini pia yale aliyotujulisha Mtume wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa Mwenyezi Mungu anashuka katika mbingu za dunia kila usiku katika thuluthi ya mwisho na kusema; "Nani mwenye kuomba nimkubalie, nani mwenye kuniomba nimpe, nani mwenye kuniomba maghfira nimghufirie."
(Alipoulizwa Imam Shafi;
'Vipi Mwenyezi Mungu anashuka?'
Akajibu;
'Kweni vipi alipanda?')
Na tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu atakuja Siku ya Kiama kuwahukumu viumbe vyake.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Sivyo hivyo! Itakapo vunjwa ardhi vipande vipande. Na akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu. Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini?".
Al Fajr – 21 – 22
Atakavyo Mwenyezi Mungu 'Irada';
Tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu anatenda atakavyo.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Atendaye ayatakayo."
Al Buruj – 16
Na tunaamini kuwa zipo Irada namna mbili.
Ya kwanza anatujulisha katika kauli Yake;
"Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda wasingeli pigana (Lau shaa'a Llahu). Lakini Mwenyezi Mungu hutenda atakavyo."
Al Baqarah – 253
Na hapa maana yake ni kutaka,
"Wala nasaha yangu haikufaini kitu nikitaka kukunasihini, ikiwa Mwenyezi Mungu anataka (Law yuriydu Llahu) kukuachieni mpotee."
Hud – 34
Na uwezo mwingine ni wa kisheria, na hamtakii isipokuwa anayempenda,
"Na Mwenyezi Mungu anataka (Yuriydu Llahu) kukurejezeni kwenye ut'iifu wake, na wanao taka kufuata matamanio wanataka mkengeuke makengeuko makubwa."
(Na maana yake hapa ni kuwa 'Hivi Ndivyo Anavyotaka Mwenyezi Mungu' lakini kakupeni uhuru wa kuchagua wenyewe mnakotaka kwenda.)
An Nisaa – 27
Na tunaamini kuwa atakacho Mwenyezi Mungu katika mambo ya kilimwengu na ya kisheria yote ni katika hekima Yake, na hafanyi kitu bila ya kuwa na hekima kubwa ndani yake, na sisi huenda tukaijuwa hekima hiyo au tusiijuwe kutokana na upungufu wa akili zetu.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote?"
At Tiyn - 8
Na akasema;
"Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?"
Al Maidah - 50
Kupenda;
Na tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala anawapenda wacha Mungu wake wanaompenda.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu."
Al Imran – 31
Na akasema;
"Basi Mwenyezi Mungu atakuja leta watu anao wapenda nao wanampenda."
Al Maidah – 54
Na akasema;
"Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanao subiri."
Al Imran – 146
Na tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu huridhika zinapofuatwa sheria zake na huchukizwa zisipofuatwa.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Mkikufuru basi Mwenyezi Mungu si mwenye haja nanyi, lakini hafurahii kufuru kwa waja wake."
Az Zumar – 7
Na akasema;
"Lakini Mwenyezi Mungu kachukia kutoka kwao, na kwa hivyo akawazuia na ikasemwa: Kaeni pamoja na wanao kaa!"
Na tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu huridhika na wale wanaoamini na kufanya mema.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Mwenyezi Mungu yu radhi nao, na wao waradhi naye. Hayo ni kwa anaye mwogopa Mola wake Mlezi."
Na tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu anamkasirikia kila mwenye kustahiki kukasirikiwa katika makafiri na wasiokuwa makafiri.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Wanao mdhania Mwenyezi Mungu dhana mbaya. Utawafikia mgeuko mbaya, na Mwenyezi Mungu awakasirikie."
Al Fat-h – 6
Na akasema;
"Lakini aliye kifungulia kifua chake kukataa - basi hao ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ipo juu yao, na wao watapata adhabu kubwa."
An Nahl – 6
Uso wa Mwenyezi Mungu;
Na tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu anao uso wenye utukufu na ukarimu.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Inabaki dhati ya Mola wako (Wajhu rabbika) yenye utukufu na ukarimu."
Al Rahman – 27
Mikono
Tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu anayo mikono miwili mitukufu.
Mwenyezi Mungu anasema;
"
Al Maidah – 64
Na akasema;
"Na wala hawakumhishimu Mwenyezi Mungu
Az Zumar – 67
(Siku ya Ridhwan Waislamu walipofungamana na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) chini ya mti kwa kumpa mkono wote kwa pamoja, mmoja baada ya mwengine, na Mwenyezi Mungu akateremsha kauli Yake;
"Bila Shaka wale wanaofungamana nawe, kwa hakika wanafungamana na Mwenyezi Mungu. Mkono wa Mwenyezi Mungu uko juu ya mikono
Al Fat-h – 10
(Ieleweke kuwa Mwenyezi Mungu anaposema anayo mikono au macho, haina maana kuwa mikono yake ni sawa na mikono yetu, au macho yake ni sawa na macho yetu - Astaghfirullah. Meza inayo miguu na viti vina miguu, lakini miguu ya viti na ya meza ni tofauti na miguu ya mwanadamu aloitengeneza meza ile, kwani sifa ya mtengenezaji lazima iwe tofauti na sifa ya kilichotengenezwa, ama sivyo mtengenezani na kilichotengenezwa watakuwa kitu kimoja. Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kupigiwa mifano bora, sifa Zake Subhanahu wa Taala haziwezi kufananishwa na sifa zetu. Lakini wakati huo huo lazima tukikubali kila alichojinasibisha nacho Subhanahu wa Taala.)
Macho
Na tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu anayo macho mawili kikweli, na hii inatokana na kauli Yake Subhanahu wa Taala aliposema kumwambia Nuh (as);
"Na unda jahazi mbele ya macho yetu na kwa mujibu wa ufunuo wetu."
Hud – 37
Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema;
"Pazia yake ni nuru, na lau
Na alipokuwa akihadithia juu ya Adajjal alisema;
"Dajjal ana chongo na Mola wenu hana chongo."
Na tunaamini kuwa macho yetu hayamfikii kumuona Mwenyezi Mungu.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Macho hayamfikilii, bali Yeye anayafikilia macho. Naye ni Mjuzi, Mwenye khabari."
Al An Am – 103
Na tunaamini kuwa Waislamu watamuona Mola wao Siku ya Kiama.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Zipo nyuso siku hiyo zita ng'ara. Zinamwangallia Mola wao Mlezi."
Al Qiyamah – 22-23
Na tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala hana mfano wake katika ukamilifu wa sifa zake.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Hapana kitu
Al Shuura – 11
Na tunaami kuwa Mwenyezi Mungu hashikwi na usingizi wala halali.
Mwenyezi Mungu anasema'
"Hashikwi na usingizi wala kulala."
Al Baqarah – 255
Na tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu hamdhulumu mtu, na hii inatokana na ukamilifu wa uadilifu Wake Subhanahu wa Taala, na kwamba hapana asichokijuwa katika matendo ya waja Wake, na kwamba hashindiwi na chochote, kwani anapotaka chochote kiwe hukiambia tu; 'Kuwa' na kikawa.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Hakika amri yake anapo taka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa."
Yasin – 82
Na tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu haguswi na machofu wala tabu ya aina yoyote ile.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Na bila ya shaka Sisi tumeziumba mbingu na ardhi na vilio baina
Qaf – 38
Na tunakiamini kila alichojithibitishia nafsi yake, akasema kuwa Anacho, basi sisi tunaamini kuwa anacho kwa uhakika, na tunaamini pia kila alichotujulisha Mtume wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya Mola wake, katika Majina Yake mazuri mazuri na Sifa Zake njema.
Lakini tunakataa mambo mawili, nayo ni;
Kufananisha (kushabihisha). Nako ni kutamka kwa ulimi au kwa moyo kuwa wasfu wa Mwenyezi Mungu unafanana na wasfu wa viumbe vyake.
Na pia tunakataa kukisia. Nako ni kujisemeza moyoni au kutamka kwa ulimi kuzikisia sifa za Mwenyezi Mungu kuwa labda ni hivi au vile.
Na tunakanusha kila Mwenyezi Mungu alichojikanushia nafsi Yake, au kile alichokikanusha Mtume wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na tunakinyamazia kila Alichokinyamazia, na tunaamini kuwa hii ndiyo njia sahihi, kwani kila alichojikanushia nafsi yake ni habari kutoka Kwake, na Yeye Subhanahu wa Taala ndiye mwenye kuijuwa nafsi Yake na ndiye Msema kweli kupita wote, Mwenye mazungumzo bora kupita wote, waja wake hawana uwezo wa kujuwa chochote juu Yake bila Yeye kuwajulisha.
Tanbih;
Kila tulichokitaja katika sifa za Mwenyezi Mungu, iwe kwa urefu au kwa ujumla, katika kuthibitisha au katika kukanusha, yote tumeyanukuu kutoka katika kitabu cha Mwenyezi Mungu (Qurani) au mafundisho ya Mtume wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) (Sunnah) iliyo sahihi nayo pia ni itikadi waliyokuwa nayo Maimamu wetu wema waliotangulia.
Tunaona kuwa inawajibika kuzifasiri nassi (dalili) zilizomo ndani ya qurani kwa uhakika wake kama anavyozistahiki Mwenyezi Mungu, na tunajitenga mbali na njia ya wageuzaji wa maana wale waliozigeuza maana na kuzifasiri kwa njia asiyoitaka Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala, na tunajitenga mbali na njia ya wabadilishaji waliobadilisha, mbali na maana iliyokusudiwa, na pia tunajitenga mbali na wazidishaji waliozidisha na kuzifanya sifa zake kuwa ni za kumfananisha.
Tuna hakika kuwa yale yaliyomo ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu na ndani ya mafundisho ya Mtume wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni haki isiyopingana, na hii inatokana na kauli Yake Subhanahu wa Taala aliposema;
"Hebu hawaizingatii hii Qur'ani? Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani yake khitilafu nyingi."
An Nisaa – 82
Na kwa vile kauli zinazopingana huwa zinasutana, na hili ni jambo lisiliowezekana katika habari anazotupa Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala na anazotupa Mtume wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na yeyote anayedai kuwa ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu au ndani ya mafundisho ya Mtume wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yamo maneno yanayopingana, akasema hayo kwa kukusudia au kwa vile moyo wake umekwenda upande, basi huyo anatakaiwa atubu kwa Mola wake na atoke ndani ya upotofu wake.
Na yeyote anayedhani kuwa mna upungufu wowote ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu au ndani ya mafundisho ya Mtume wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) au baina
"Tumeamini, zote zimetoka kwa mola wetu."
Aali Imran – 7
Na ajuwe ya kuwa Qurani na Sunnah haviwezi kugongana wala kupingana wala hapana hitilafu baina yake.
Mlango;
Na tunaamini juu Malaika wa Mwenyezi Mungu kama ulivyokuja wasfu wao ndani ya Qurani kwamba wao ni;
"
Mwenyezi Mungu amewaumba ili wamuabudu na kumtii.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Hawafanyi kiburi wakaacha kumuabudu, wala hawachoki.
Wanamtakasa usiku na mchana, wala hawanyong'onyei."
Al Anbiya – 19 – 20
Mwenyezi Mungu akatujaalia tusiweze kuwaona, na aliwafanya wengine kati ya waja wake kuweza kuwaona, kwani Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuona Jibril akiwa katika umbile lake la kweli ana mbawa mia sita, akiwa ameizinga anga yote juu yake.
Jibril (as) aliwahi pia kuonekana na Bibi Maryam akiwa katika umbile la binadamu aliyekamilika, akazungumza naye, na aliwahi pia kumjia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa pamoja na Masahaba wake (Radhiya Allaahu ‘anhm) akiwa katika umbile la mwanamume asiyejulikana wala hapakuwa na ishara yoyote usoni mwake kama ni mtu aliyetoka safari ndefu, akaliegemeza goti lake juu ya goti la Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kuuweka mkono wake juu ya paja la Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kisha akazungumza naye huku Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akimjibu, na baada ya kuondoka ndipo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawaambia Masahaba wake (Radhiya Allaahu ‘anhm) kuwa yule alikuwa ni Jibril.
Na tunaamini kuwa Malaika wana kazi zao maalum walizopewa na Mola wao. Jibril ni mletaji wahyi kwa Mitume, anawateremshia kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kuwafikishia anaotumwa kuwafikishia katika Mitume yake Subhanahu wa Taala. Na yupo Mikail (as) aliyepewa kazi ya kuteremsha mvua na ya mazao anapopewa amri na Mwenyezi Mungu. Na yupo Israfil mwenye kazi ya kupuliza parapanda (baragumu) siku ya Kiama. Na yupo Malaika wa kifo aliyepewa kazi ya kuzitoa roho wakati wa kufa, na yupo Malaika wa majabali, na yupo Malik mlinzi wa mlango wa Motoni, na wapo Malaika wanaowashughulikia watoto wachanga matumboni mwa mama zao, na weginge waliopewa kazi ya kuwahifadhi wanadamu na wengine wenye kuandika amali zao, na kila mtu ana Malaika wawili.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Wanapo pokea wapokeaji wawili, wanao kaa kuliani na kushotoni
Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari (kuandika)."
Qaf – 17 – 18
Na wengine wana kazi za kuwauliza maiti baada ya kufikishwa kaburini, wanajiwa na Malaika wawili na kumuuliza Nani Mola wake, nini dini yake, nani mtume wake?
Mwenyezi Mungu anasema;
"Mwenyezi Mungu huwatia imara wenye kuamini kwa kauli ya imara katika maisha ya dunia na katika Akhera. Na Mwenyezi Mungu huwaacha kupotea hao wenye kudhulumu. Na Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo."
Ibrahim – 27
Na wapo Malaika waliopewa kazi ya kuwashughulikia watu wa Peponi.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Na Malaika wanawaingilia katika kila mlango.
(Wakiwaambia) Assalamu Alaikum! Amani iwe juu yenu, kwa sababu ya mlivyo subiri! Basi ni mema mno malipo ya Nyumba ya Akhera."
Al Raad – 23 – 34
Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitujulisha kuwa ndani ya 'Baitul Maamur', iliyopo mbinguni wanaingia na kusali ndani yake kila siku Malaika elfu sabini wakishamaliza hawaipati fursa ya kurudi humo tena.
Mlango;
Na tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu amewateremshia Mitume yake vitabu ili viwe hoja na mwangaza kwa walimwengu kwa ajili ya kuwafundisha hekima na kwa ajili ya kuwatakasa.
Na tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu amemteremshia kila Mtume kitabu.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Kwa hakika tuliwatuma Mitume wetu kwa dalili waziwazi, na tukateremsha Kitabu pamoja nao na Mizani, ili watu wasimamie uadilifu."
Al Hadid – 25
Na katika vitabu hivyo tunavyovijuwa ni;
1 - Taurati ; Mwenyezi Mungu alimteremsia Nabii Musa (as), na hiki ni kitabu kitukufu kupita vyote vya Bani Israil.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Hakika Sisi tuliteremsha Taurati yenye uwongofu na nuru, ambayo kwayo Manabii walio nyenyekea kiislamu, na wachamngu, na
