Mwandamo Wa Mwezi, Kila Mji Ufuate Mwezi Unapoonekena Kwao Au Mwandamo Wa Kimataifa?
SWALI
Nimesikia kupitia radio times na radio Quran kupitia masheik maarufu wa bakwata wakisema wanao warka uliosambazwa na mufti wa saudia kwamba kila sehemu wafunge kwa kufata mwez wa sehem zao, vipi hamkubaliani na warka huo kuwepo? Ama hamkubalian na mufti huyo kwa sababu zipi? Ukizingatia hapo ndio mahala patakatifu zaidi?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako hili. Ingekuwa vyema
Kauli hii ya Shaykh haifuatwi wala haitolewi na wenye mrengo mmoja. Nchi za
Je, hao mashekhe maarufu wa Bakwata katika waraka huo walitoa swali aliloulizwa Shaykh Ibn Baaz au walitoa sehemu ya jibu wanayotaka iunge msimamo wao tu? Kwetu sisi tunawaheshimu
Kwa kweli tunaona ajabu kwa mashekhe hao wa serikali wanaotoka mbelembele kwenye vyombo vya habari walivyopewa kutumia na kupotosha watu kwa kuchukua kauli hiyo pekee kutoka kwa Shaykh Ibn Baaz lakini wakaacha kufuata yale maelekezo mengine ya Shaykh Ibn Baaz ya kukataza kusoma Khitmah, Mawlid na kuacha kufuata Bid‘ah nyinginezo ambazo hao mashekhe wa serikali wanazifanya na kuzieneza?
Tufahamu kuwa msimamo wa Muislamu yeyote unatakiwa uwe ni kufuata haki na ukweli. Ikiwa Shaykh Ibn Baaz amesema hivyo na kwa ibara yake hapo juu wawaachie Mashaykh wa nchi hiyo waamue, amewapatia Mashaykh wa sehemu zao watazame ukweli na haki. Lakini hata hivyo wapo Mashaykh wengi waliosema kuwa kufuatwe mwandamo wa kimataifa na hiyo ndio kauli ya Jamhuur (wanachuoni wengi). Msimamo huu ndio muono wa madhehebu ya Imaam Abu Haniyfah, Maalik, na Ahmad bin Hanbal. Wengine wenye msimamo huu ni Ibn Taymiyah, Ibn Qudaamah al-Maqdisiy,, ash-Shawkaaniy, Dkt. Yusuf al-Qaradhwaawiy, Dkt. Ahmad Shaakir, Dkt. Wahbah az-Zuhayliy, al-Qaanujiy, ‘Abdur-Rahman al-Juzairiy na pia Sayyid Saabiq. Na kwa upande wa dalili, rai hii ya kufuata mwezi wa kimataifa una nguvu zaidi kuliko kufuata mwezi wa nchi.
Tazama masuala hayo kwenye vitabu vya Fiqh vya kutegemewa
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


