Skip navigation.
Home kabah

Mchuzi Wa Kima Na Mayai

 

Vipimo

Nyama ya kusaga                          2 LB (Ratili)

Mayai                                              6

Vitunguu                                         4

Thomu na Tangawizi                      1 Kijiko cha supu

Pilipili mbichi iliyosagwa                 1 Kijiko cha chai

Nyanya iliyokatwa katwa               4

Kotmiri                                          ½ Kikombe

Pilipili Manga                                  ¼Kijiko cha chai

Bizari ya curry                               ½ Kijiko cha chai

Nyanya ya kopo                            3 Vijiko vya supu

Garam masala                               1 Kijiko cha supu

Mafuta ya kukaangia                     Kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

  1. Chemsha mayai, yakiiva ambua maganda na uweke kando.
  2. Katika sufuria weka mafuta yapate moto, Kaanga vitunguu hadi vigeuke na kuwa rangi ya hudhurungi.
  3. Halafu tia thomu na tangawizi kanga kidogo tu, kisha tia bizari zote na pilipili uendelee kukaanga.
  4. Kisha weka nyama na uiache motoni huku unakoroga hadi iwe si nyekundu tena.
  5. Tia nyanya na chumvi ziache zilainike halafu tia nyanya ya kopo.
  6. Ongeza maji kiasi unavyopenda mchuzi wako kuwa mzito au mwepesi.
  7. Kisha weka yale mayai ya kuchemsha na iache itokote kidogo kwa moto mdogo.
  8. Mwishoe mwagia kotmiri, changanya na umimine katika bakuli na itakuwa tayari kwa kuliwa na wali au mkate upendayo.