Skip navigation.
Home kabah

Mambo Ya Kufanya Siku Ya Ijumaa

12 Rabiy'ul Aakhir 1426 20-05-2005

 

Ijumaa hii tunamalizia kuelezea utukufu wa siku hii kwa kuelezea mambo yanayotupasa kuyafanya yenye fadhila  na thawabu nyingi.  

Kukoga (Ghuslu) ni wajibu

 

حديث أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: الْغُسْلُ يَوْمَ الْجُمُعَةِ وَاجِبٌ عَلَى كُلِّ مُحْتَلِمٍ ( أخرجه البخاري) 

Kutoka kwa Abi Sa'iid Al-Khudhriy ambaye alisema: Mtume صلى الله عليه وسلم  kasema  Ghuslu ( kukoga kwa kujitia tohara) siku ya Ijumaa ni wajibu kwa kila Muislamu aliyebaleghe.  (Al-Bukhari)

Inapendekezwa kwa kila anayekwenda kuswali  kujisafisha, kupiga mswaki, kujitia mafuta mazuri (isipokuwa mwanamke) na kuvaa nguo iliyo nzuri kabisa.  Muislamu akitimiza adabu ya Swala ya Ijumaa hufutiwa madhambi yake  ya wiki .   

عن سلمان رضي الله عنه قال: قال رسول الله  صلى الله عليه  وسلم   لا يغتسل رجل يوم الجمعة، ويتطهر ما إستطاع من طهر، ويدّهن من دهنه، أو يمس من طيب بيته، ثم يخرج فلا يفرق بين إثنين، ثم يصلي ما كتب له، ثم ينصت إذا تكلم الإمام، إلا غفر له ما بينه وبين الجمعة الأخرى) رواه البخاري(

Kutoka kwa Salmaan رضي الله عنه  ambaye alisema:  Kasema Mtume صلى الله عليه وسلم "Muislamu atakayekoga (Ghuslu)  siku ya Ijumaa, akajisafisha vizuri awezavyo, akatia rangi (sio nyeusi)   (nywele zake),  au akajipaka mafuta mazuri  aliyonayo nyumbani kwake, kisha akaenda msikitini bila ya kufarikisha (kuwapangua akipita) watu wawili (ambao wameshakaa kitako msikitini), akaswali aliyofaridhishwa, kisha akasikiliza  (khutba) kimya, hufutiwa madhambi yake yaliyo baina ya Ijumaa hiyo na ijumaa ijayo.    (Imehadithiwa na Al-Bukhari na Imam Ahmad).

 

Swala ya Ijumaa 

  Allaah سبحانه وتعالى Ametuamrisha kwenda kuswali Swali ya Ijumaa

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِي لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَى ذِكْرِ اللَّهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ذَلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ

{Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua}  (Al-Jumua  62:9 )

Ni wajibu kwa kila mwanamme Muislamu kwenda kuswali Ijumaa,  na hatari ya  kutokwenda kuswali bila ya kuwa na sababu iliyoruhusu sheria  ni kuwa  Allaah سبحانه وتعالى  humpiga muhuri mtu  moyoni  mwake, kama katika hadithi sahihi ifuatayo:

 قال رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: من ترك ثلاث جمع تهاونا طبع الله على قلبه – (رواه أحمد وأصحاب السنن،)   

{ Kasema Mtume صلى الله عليه وسلم : Atakayewacha (kuswali swala ya) Ijumaa mara tatu bila ya sababu yeyote, Allaah سبحانه وتعالى humpiga muhuri katika moyo wake}  (Imehadithiwa na Ahmad na jamaa wa Sunna )

Kupigwa muhuri huo inamaanisha kwamba Allaah سبحانه وتعالى Ameshampa chapa huyu mtu kuwa ni 'asi na amekwishatumbukia katika makemeo ya Allaah سبحانه وتعالى  kwamba    ni katika walioghafilika  kama alivyotutahadharisha Mtume صلى الله عليه وسلم

حديث ابن عمر وأبي هريرة رضي الله عنهما المخرج في صحيح مسلم من أنهما سمعا رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول على أعواد منبره: لينتهين أقوام عن ودعهم الجمعات أو ليختمن الله على قلوبهم ثم ليكونن من الغافلين

Kutoka kwa Ibn 'Umar na Abu Hurayra رضي الله عنهما kwamba wamemsikia Mtume صلى الله عليه وسلم akisema : Wasiohudhuria  Swala ya Ijumaa  wabadilishe  mtindo wao huo au sivyo Allaah سبحانه وتعالى atawapiga mihuri katika nyoyo zao  na watakuwa  miongoni wa walioghafilika.  (Imehadithiwa na   Muslim  )

Kufika mapema msikitini   

Kila atakapofika mtu mapema msikitini huwa amepata daraja Fulani na muhimu kabisa ni kufika kabla ya khutba kuanza, akichelewa mtu kufika akakosa khutba atakuwa amekosa Swala ya Ijumaa

حديث أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، أَنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: مَنِ اغْتَسَلَ يَوْمَ الْجُمُعَةِ غُسْلَ الْجَنَابَةِ ثُمَّ رَاحَ فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ بَدَنَةً، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الثَّانِيَةِ فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ بَقَرَةً، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الثَّالِثَةِ فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ كَبْشًا أَقْرَنَ، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الرَّابِعَةِ فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ دَجَاجَةً، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الْخَامِسَةِ فَكَأَنَّما قَرَّبَ بَيْضَةً، فَإِذَا خَرَجَ الإِمَامُ حَضَرَتِ الْمَلاَئِكَةُ يَسْتَمِعُونَ الذِّكْرَ (أخرجه البخاري )

Kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه ambaye alisema :  Mtume صلى الله عليه وسلم kasema;  Atakayekoga (ghuslu) siku ya Ijumaa kisha akaenda msikitini, itakuwa kama mfano ametoa (kafara ya)   ngamia.  (Qurbani)     Akienda  saa ya pili yake, itakuwa kama katoa (kafara ya) nġombe.  Akienda saa ya tatu yake, itakuwa kama katoa (kafara ya)  kondoo mwenye pembe. Akienda saa ya nne yake, itakuwa kama  katoa   kuku.  Akienda saa ya  tano yake itakuwa kama katoa   yai .  Imamu akifika, Malaika watakuwepo  kusikiliza dhikr . ( Imehadithiwa na  Al-Bukhari )

Sura za  kusoma siku ya Ijumaa

 

·        Suratul Kahf

عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه  وسلم  قال: من قرأ سورة الكهف يوم الجمعة أضاء له من النور ما بين الجمعتين     ( رواه الترمذي.)

Kutoka kwa Abu Sa'id Al-Khudhriy رضي الله عنه ambae alisema:  Kasema Mtume صلى الله عليه وسلم  :Atakayesoma Suratul-Kahf siku ya Ijumaa atakuwa katika mwangaza baina ya Ijumaa mbili.  (Imehadithiwa na  At-Tirmidhiy)

·        Swala ya Alfajiri

حديث أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، قَالَ: كَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَقْرَأُ فِي الْجُمُعَةِ، فِي صَلاَةِ الْفَجْرِ، آلَم تَنْزيلُ، السَّجْدَةَ، وَ هَلْ أَتَى عَلَى الإِنْسَانِ ( أخرجه البخاري)

Kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه ambaye      alisema:  Alikuwa Mtume صلى الله عليه وسلم           akisoma sura ya Alif-Laam-Tanziilu (Suratus Sajda) na  Hal-Ataa 'Alal-Insaan (Suratul Insaan)  (Imehadithiwa na Al-Bukhari)

·        Kumswalia Mtume صلى الله عليه وسلم

عن أوس بن أوس رضي الله عنه قال: قال رسول الله  صلى الله عليه  وسلم  إن من أفضل أيامكم يوم الجمعة، فأكثروا علي من الصلاة فيه، فإن صلاتكم معروضة علي  ) رواه أبو داود)

Kutoka kwa Aws Ibn Aws رضي الله عنه ambaye alisema:  Kasema Mtume صلى الله عليه وسلم : Siku bora kabisa kwenu ni siku ya Ijumaa, kwa hiyo zidisheni kuniswalia,  kwani Swala (kuniombea kwenu) zenu zinaonyeshwa kwangu (Imehadithiwa na Abu Dawood).

 

 ********