Skip navigation.
Home kabah

Mahitajio Ya Nafsi

Mahitajio ya miili yetu  (chakula) yote  hutoka ardhini ambako ndio asili ya kuumbwa huu mwili.

 

((الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الأََرْضَ مَهْدًا وَسَلَكَ لَكُمْ فِيهَا سُبُلاً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاء مَاء فَأَخْرَجْنَا بِهِ أَزْوَاجًا مِّن نَّبَاتٍ شَتَّى)) ((كُلُوا وَارْعَوْا أَنْعَامَكُمْ إِنَّ فِي ذَلِكَ لأَيَاتٍ لأُُوْلِي النُّهَى)) ((مِنْهَا خَلَقْنَاكُمْ وَفِيهَا نُعِيدُكُمْ وَمِنْهَا نُخْرِجُكُمْ تَارَةً أُخْرَى))

 

((Ambaye Aamekufanyieni ardhi kuwa tandiko, na Akakupitishieni humo njia, na Akakuteremshieni kutoka mbinguni maji. Na kwa hayo Tukatoa namna mbali mbali za mimema)) ((Kuleni, na mchunge wanyama wenu. Hakika katika hayo zipo ishara kwa wenye akili)) ((Kutokana nayo (ardhi) Tumekuumbeni, na humo Tunakurudisheni, na kutoka humo Tutakutoeni mara nyengine)) [Twaahaa: 53-55]

 

Nafsi hali kadhalika mahitajio yake nayo yanotakana na asili yake ambayo ni kutoka juu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala). Kwa hiyo, vitu viwili hivi visipopata mahitajio yake utaona kuwa vinadhoofika.   Mwili huenda mtu akakonda na kuumwa kwa kutokupata chakula cha siha, na nafsi ikikosa mahitaji yake ambayo ni kuwasiliana na kuambatana na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa kila aina ya ibada na dhikr, basi nayo hudhoofika ndio utamuona mtu yuko kwenye maovu tu kwa sababu nafsi yake iko mbali na Mola wake. Nafsi nyingine hata haijamtambua Mola wake. Na kwa mwenye kumjua vile vile kama sisi Waislamu tunaomuamini Allah (Subhaanahu wa Ta'ala).  ikiwa hatuipi nafsi zetu mahitajio yake ndio utamuoma mtu vile vile yuko kwenye maasi na mwengine japo hafanyi maasi lakini yuko kwenye dhiki fulani, hana raha kwa vile ameikosesha nafsi yake mahitajio yake.

 

Ibada na vitendo vyenye kuambatana na Allah (Subhaanahu wa Ta'ala):  

 

Jambo la kwanza la  kuambatana na Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) ni kuitoharisha nafsi  kwa  kuomba maghfira na kutubu.

 

Maghfira na toba

 

Kwa vile binaadamu sote ni wenye kufanya makosa kila siku kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)    

((كل بني آدم خطاء، و خير الخطائين التوابون)) حسن الألباني صحيح الجامع

 

((Kila Binaadamu ni mkosa na mkosa mbora kabisa ni yule anayeomba toba)).  [Ameipa daraja ya Hasan Shaykh Al-Baaniy  kutoka Swahihil-Jaami']   

 

Kwa Rahma ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  hata binaadamu awe ana makosa vipi, huenda akafutiwa dhambi zake zote, kwa hiyo mtu asikate tamaa au kukhofu kuwa dhambi zake hazitofutwa. 

 

 

((قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَى أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِن رَّحْمَةِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ))  

 

((Sema: Enyi waja wangu waliojidhulumu nafsi zao, msikate tamaa na Rahma ya Allaah. Hakika Allaah husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu)) [Az-Zumar: 53]

 

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)   Ametuamrisha tumuombe toba katika Aayah nyingi za Qur-aan kama mfano wa Aayah  zifuatazo:  

 

 

((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا))

 

((Enyi mlioamini! Tubuni kwa Allaah toba iliyo ya kweli))  [At-Tahriym: 8]

 

 

((وَتُوبُوا إِلَى اللَّهِ جَمِيعًا أَيُّهَا الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ))

 

((Na tubuni nyote kwa Allaah, enyi Waumini, ili mpate  kufanikiwa)) [An- Nuur: 31]

 

 

*****