Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislam - 3
Chuo Kikuu Cha California Ya Kusini
USC-MSA Muhtasari Ya Maandiko Ya Waislamu
Imefasiriwa na: ‘Abdun-Naaswir Hikmany
Suala Nambari 3 Linaloeleweka Vibaya
· sehemu ya urithi wa mwanamme ni kubwa kuliko ya mwanamke
· mwanamme anaweza kuoa mwanamke asiye Muislamu, mwanamke hawezi
· mwanamke ni lazima avae hijaab
JIBU
Suala hili pana halielekei kufuatana kwa mnasaba wa hoja zinazotolewa. Tathmini ya mwanzo na muhimu zaidi ya kuifanya ni kuhusu suala maarufu “Je wanaume ni sawa na wanawake?” Ni suala ambalo limetengenezwa vibaya, lisiloweza kujibika. Tatizo ambalo watu wengi wanatumia kuliepuka ni kutolitafsiri neno “usawa”. Hii ni nukta inayohitaji kuupambanua usawa ambao ni lazima uelezwe kwa hali inayopimika. Kwa mfano, wanawake kwa kiwango fulani wapo juu kuliko wanaume
Je, kinachofuata, ni hali gani muhimu ambayo tuna wasiwasi nayo kuhusiana na usawa wa jinsia? Kiasili, kutokana na uoni wa Qur-aan na Sunnah, hali iliyokuwa muhimu zaidi ni nani aliyekuwa mtiifu kwa Allaah, wanaume au wanawake? Suala hili bila ya shaka linajibiwa ndani ya Qur-aan (iliyotafsiriwa):
{{Na watakaofanya vitendo vizuri, wakiwa wanaume au wanawake, hali wao ni wenye kuamini, basi hao wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa hata tundu ya kokwa ya tende.}} [4:124]
{{Bila shaka wanaume wenye kufuata vizuri nguzo za Uislamu, na wanawake wenye kufuata vizuri nguzo za Uislamu; na wanaume wanaoamini vizuri nguzo za Imani, na wanawake wanaoamini vizuri nguzo za Imani; na wanaume wasemao kweli, na wanawake wasemao kweli; na wanaume wanaosubiri, na wanawake wanaosubiri; na wanaume wanaonyenyekea na wanawake wanaonyenyekea; na wanaume wanaotoa (Zakaat na) sadaka, na wanawake wanaotoa (Zakaat na) sadaka, na wanaume wanaofunga, na wanawake wanaofunga; na wanaume wanaojihifadhi tupu zao, na wanawake wanaojihifadhi; na wanaume wanaomtaja Mwenyezi Mungu (kwa wingi), na wanawake wanaomtaja Mwenyezi Mungu (kwa wingi) Mwenyezi Mungu Amewaandalia msamaha na ujira mkubwa.}} [33:35]
Qur-aan na Sunnah zinarudia tena na tena kwamba Allaah Anampendelea mtu mmoja dhidi ya mtu mwengine kwa kigezo chake cha hamasa, unyenyekevu, khofu, mapenzi, na matarajio ya Allaah (neno la kiarabu la ‘Taqwa’ ‘ucha Mungu’ ni gumu kulipatia tafsiri yake halisi). Sifa nyengine zote zimetenguliwa: jinsia, kabila, taifa, asili, n.k.
Kwa vile Allaah Hapendelei jinsia moja dhidi ya nyengine ndani ya matakwa Yake kwetu sisi (na inasaidia kukumbuka kwamba Allaah sio mwanamume wala mwanamke), na sasa tunaweza kuelezea tofauti baina ya jinsia ndani ya Uislamu.
Kwanza, wanaume na wanawake hawapo sawa kama tunavyoelewa. Muumba Anaelezea ndani ya Qur-aan (iliyotafsiriwa):
{{…na mwanamume si sawa na mwanamke…}} [3:36]
Wanaume na wanawake ni tofauti kwenye tabia, na kwenye majukumu
{{Na waozeni wajane miongoni mwenu (waungwana), na walio wema katika watumwa wenu (wanaume) na wajakazi wenu, kama watakuwa mafakiri Mwenyezi Mungu Atawatajirisha katika fadhila Zake; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua}} [24:32]
Ndani ya Aayah hii, Muumba Anatilia mkazo kwamba ndoa ni lazima ifungwe mapema na Waislamu: tabia ya kuwa pweke isikuwepo. Kwa kuwepo hili akilini, tunaweza kuanza kuelewa hoja nne zilizotajwa hapo juu kwa hitimisho lisilo na kosa lolote.
Wanaume na wanawake ni tofauti kwenye kuwajibika kwao kwa familia ambazo wanahimizwa
{{Wanaume (wawe) ni walinzi wa wanawake; kwa sababu Mwenyezi Mungu Amewafadhilisha baadhi
Kutokana na Sunnah, hususan ndani ya somo la Sunnah linaloitwa Swahiyh al-Bukhaariy, tunaona:
Amesimulia ‘Amr bin Al-Haarih: Zaynab, mke wa ‘Abdullaah alisema: “Nilikuwa Msikitini nikamuona Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ‘Enyi wanawake! Toeni sadaka hata kama kutoka kwenye mapambo yenu’ Zaynab alikuwa akimpatia ‘Abdullaah na mayatima walio chini ya hifadhi yake. Hivyo alimwambia ‘Abdullaah, “Je unaweza kumuuliza Mtume wa Allaah iwapo naweza kutumia sehemu ya Zakaat kwako na mayatima walio chini ya hifadhi yangu?” Alijibu “Je, utamuuliza mwenyewe Mtume wa Allaah?” (Zaynab akaongeza): Hivyo nilienda kwa Mtume na hapo nikamuona mwanamke wa ki-Aanswari aliyekuwa amesimama mlangoni (kwa Mtume) aliyekuwa na tatizo lililo sawa na langu. Bilaal alipita mbele yetu na tukamuomba, “Muulize Mtume wa Allaah iwapo naweza kutumia sehemu ya Zakaat kwa mume wangu na mayatima walio chini ya hifadhi yangu” Na tukamuomba Bilaal kutomtaarifu Mtume kuhusu sisi. Hivyo Bilaal aliingia ndani na kumuuliza Mtume kuhusiana na tatizo letu. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliuliza, “Hao wawili ni kina nani?” Bilaal alijibu kwamba alikuwa ni Zaynab. Mtume alisema, “Zaynab gani?” Bilaal alisema, “Mke wa ‘Abdullaah (bin Mas’uud)”. Mtume akasema, “Ndio, (inawezekana kwake), na atapata malipo mara mbili yake (kwa tendo hilo): Kwanza kwa kusaidia jamaa zake, na pili kwa kutoa Zakaat.”
Kutokana na waume kulazimishwa kuwahudumia wake, na kwamba ndoa ni pendekezo lililotiliwa mkazo (
{{Na wapeni wanawake mahari
Allaah Anasema ndani ya Qur-aan (iliyotafsiriwa):
{{… Nao (wanawake) wanayo haki kwa Sharia (kufanyiwa na waume zao) kama ile haki iliyo juu
Hali hii haimuathiri (hata chembe) wadhifa wa Muumba ambaye Ameeleza kwamba Hawaangalii wanawake kuwa ni bora Kwake kuliko wanaume, au kinyume chake. Isipokuwa kwa njia nyepesi ya kugawa majukumu ndani ya nyumba yenye watu wazima wawili: mtu mmoja ni lazima awe na kauli ya mwisho katika masuala ya kila siku.
Wakati wanaume wanaruhusiwa kuoa hadi wake wanne, pia wanalazimika kabla yake kutimiza masharti ya kuweza kuwahudumia kifedha. Pia wamtumikie kila mke kwa haki na usawa pamoja na majukumu ya ndoa na uchumi. Allaah Anasema ndani ya Qur-aan (iliyotafsiriwa):
{{Na
Juu ya hivyo, wanawake wanaruhusiwa kukataa posa yoyote iliyofanywa kwake na mposaji aliye tayari (kuoa), hivyo kama atahisi kwamba hawezi kutimiza kanuni za Qur-aan na Sunnah ikiwa ataolewa na mtu fulani, anaweza kukataa posa yake (mposaji). Ingawa (tuhuma hizi) si sahihi kwa Uislamu, ni vyema ikabainishwa kwamba dini zote mbili; Uyahudi na Ukristo unakubali ndoa ya mke zaidi ya mmoja. Fikra hii sio kwamba ni ngeni kwa wasiokuwa Waislamu kama inavyodaiwa.
Mwisho, uvaaji wa hijabu kwa wanawake ni jambo lisilo na mantiki kudai kwamba wanawake wapo chini kuliko wanaume. Ni bora kuikemea jamii inayokubali picha za uchi pornography kuliko kuikemea jamii inayokubali hijabu. Ikiangaliwa kwamba Allaah sio mwanamume wala mwanamke, na ikiangaliwa kwamba Hawatukuzi watu Kwake kwa kigezo cha jinsia zao, ikiangaliwa kwamba Muumba Anatujali sote wanaume kwa wanawake, ikiangaliwa kwamba shahawa za kimwili na shinikizo la mahitaji ya wanaume yapo juu kuliko yale ya wanawake….yakiangaliwa yote haya, basi hakuna maana yoyote kuvurumisha maelezo mabaya kwenye kanuni inayofuata iliyomo ndani ya Qur-aan (iliyotafsiriwa):
{{Waambie Waislamu wanaume wainamishe macho yao (wasitazame yaliyokatazwa), na wazilinde tupu zao, hili ni takaso kwao; bila shaka Mwenyezi Mungu Anazo habari za (yote) wanayoyafanya. Na waambie Waislamu wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasidhihirishe viungo vyao isipokuwa vinavyodhihirika (nao ni uso na vitanga vya mikono). Na waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao, na wasionyeshe mapambo yao ila kwa waume zao….}} [24:30-31]
{{Ewe Mtume! Waambie wake zako, na binti zako, na wanawake wa Kiislamu (wengine – waambie) wajiteremshie uzuri nguo zao. Kufanya hivyo kutapelekea upesi wajulikane (kuwa ni watu wa hishima ili) wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu.}} [33:59]
Kwenye suala hili linaloeleweka vibaya, kuna maelezo marefu ya kuendelea kuandika, mengi
Itaendelea inshaAllaah...
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
