Hadiyth Ya 08 - Nitamsibu Mja Wangu Kwa Homa Duniani Nimpunguzie Moto Wa Akhera
Hadiyth Ya 8
Nitamsibu Mja Wangu Kwa Homa Duniani Nimpunguzie Moto Wa Akhera
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ عَادَ مَرِيضًا وَمَعَهُ أَبُو هُرَيْرَةَ مِنْ وَعْكٍ كَانَ بِهِ فَقَالَ لَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((أَبْشِرْ. إِنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ يَقُولُ: نَارِي أُسَلِّطُهَا عَلَى عَبْدِي الْمُؤْمِنِ فِي الدُّنْيَا لِتَكُونَ حَظَّهُ مِنْ النَّارِ فِي الْآخِرَةِ)) أحمد وابن ماجه والترمذي – حديث حسن
Kutoka kwa Abu Hurayrahرضي الله عنه kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم alimtembelea mgonjwa aliyekuwa na homa pamoja naye akamwambia mgonjwa: ((Bishara njema (Furahi) kutoka kwa Allaah Anasema: Nitamsibu mja Wangu duniani kwa kwa moto (homa) Wangu ili aepukane na sehemu ya moto wa Akhera)) [Ahmad, Ibn Maajah, At-Tirmidhiy- Hadiyth Hasan]
- Login or register to post comments
- Email this page


