Skip navigation.
Home kabah

Kauli Ya Swahaba Juu Ya Baadhi Ya Aya Katika Qur'aan

21 Rajab 1426 26-08-2005

 

Aya tulizozitaja kuhusu nafsi itakavyojuta kwa kusema 'Ya hasrataa" (Ee majuto yangu) ambazo ziko  katika Suratuz-Zumar zimetangulizwa na  aya ambao ni aya ya pekee katika Qur'aan nzima yenye kutia matumaini baada ya mwanaadam kukosea nayo ni:

}}قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَى أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِن رَّحْمَةِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ{{

{{Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu}} Az-Zumar: 53 

Imetoka kwa Shutayr bin Shakal ambaye kasema kwamba; Nimemsikia Ibn Ma'suud رضي الله عنه   akisema;   

 Aya tukufu kabisa katika kitabu cha Allaah سبحانه وتعالى  ni

}}اللّهُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّوم{{ 

{{Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele}}  Al-Baqarah: : 255

 

Aya iliyokuwa na ufafanuzi kabisa kuhusu mazuri na maovu ni;

}}إِنَّ اللّهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالإِحْسَانِ{{

{{Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani}} An-Nahl:90

 

Aya yenye kuonyesha matumaini makubwa kabisa ni:

}}قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَى أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِن رَّحْمَةِ اللَّه{{

{{Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu}} Az-zumar:53

 

Aya iliyokuwa ni dhahiri kabisa katika kumtegemea Allaah سبحانه وتعالى ni:

}}وَمَن يَتَّقِ اللَّهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا{{

}}وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ{{

{{Na anaye mcha Mwenyezi Mungu humtengezea njia ya kutokea}}

{{Na humruzuku kwa jiha asiyo tazamia}} At-Talaaq: 2-3

Masruuq akamwambia (Shutayr bin Shakal); Umesema kweli (kwamba kauli hiyo kasema Ibn Mas'uud رضي الله عنه )

(At-Tabaraniy 9:142)

 

 *********