Kurudisha Ubikra Haifai Na Ni Udanganyifu

SWALI:

Nimesoma nakala yenu, nimevutiwa sana na ushauri wenu. lakini kama ilivyo kwa wanaume zipo dawa za kienyeji za kuongeza uume ambazo hazina madhara. sasa naomba kuuliza hakuna dawa  za kienyeji za kuweza kurudisha bikira ambazo  hazina madhara? Tafadhali naomba unijibu kwenye email  yangu. asanteni   sana

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa dada yetu muuliza swali. Hakika ni kuwa zipo dawa za kienyeji za kurudisha ubikira bandia. Hapa lakini tunataka kuuliza kwa nini mwanamke wa Kiislamu anataka kurudisha ubikira? Hii ni njia ya udanganyifu inayotumiwa na wasichana wanaoolewa hasa kwa siku hizi . Kwa nini wanafanya hivyo? Wao wanafanya hivyo ili kuwadanganya ma-bwana harusi kwa ule usiku wa mwanzo kuwa wao bado ni watahirifu na wamejihifadhi kutokana na zinaa. Wenye kufanya hayo aghalabu huwa wamezunguka na wanaume wengine kabla ya ndoa katika kitendo cha zinaa. Mume anadhania kwa usiku huo wa mwanzo kuwa mkewe ni bikira naye ni wa mwanzo kufungua kizibo ilhali si hivyo.

 

Ikiwa tayari umeolewa na unaishi na mumeo unatakia nini tena ubikira kwani ubikira ni kama ujana unapopita haurudi tena baada ya kukutana na mumeo.

 

Tutahadharini hayo kwani Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

" Mwenye kutughushi sisi (kutudanganya) si katika sisi" (Muslim).

 

Na tufahamu kuwa udanganyifu ni alama moja ya unafiki.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

Share