Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislam - 10
Chuo Kikuu Cha California Ya Kusini
USC-MSA Muhtasari Ya Maandiko Ya Waislamu
Imefasiriwa na: ‘Abdun-Naaswir Hikmany
Suala Nambari 10 Linaloeleweka Vibaya
Uislamu unazalisha jamii iliyo vivu, isiyoelimika kwasababu:
- vitu vyote vinatokana na Mungu, na hivyo ni sawa kuamini hakuna hiari ya mwanaadamu-‘fatalism’
- teknolojia na sayansi ya sasa haikubaliwi
Hoja zilizotolewa kwa suala hili linaloeleweka vibaya ni za uongo, na
{{Na wale washirikina wanasema: “
{{Na husema: “Angalipenda Mwingi wa rehema tusingewaabudu hao (masanamu, Ametuandikia Mwenyewe haya Mwenyezi Mungu, basi Anayapenda).” Hawana ilimu kwa haya (wanayoyasema); hawasemi ila maneno ya kuvurumiza tu.}} [43:20]
Allaah Ametufundisha kupitia kwa Qur-aan na Sunnah kwamba sote tuna kiwango fulani cha uhuru. Uhuru huu ni lazima ufanyiwe kazi sawa sawa kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah ili kumridhisha Muumba. Hii ni hamasa iliyo kubwa kwa Waislamu wote kuwasukuma kuwa ni wenye ujuzi ulio bora, wanaweza kuwa Waislamu walio imara kabisa. Kama jamii ya Waisalmu leo hawawezi kusuluhisha matatizo
Kutokana na Sunnah, hususan ndani ya somo la Sunnah linaloitwa Sunnah ya Abuu-Daawuud, tunaona:
Amesimulia Anas bin Maalik: Mtu wa Answaar alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kumuomba, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuuliza: Jee una chochote ndani ya nyumba yako? Akajibu: Ndio, kipande cha nguo, sehemu ambayo tunavaa na sehemu ambayo tunatandika (katika sakafu), na bakuli la mbao ambalo tunakunywia maji. Alisema: Vilete kwangu. Baadaye alivileta vitu hivi kwake na yeye (Mtume) alivichukua kwenye mkono wake na kuuliza: Ni nani atakayevinunua hivi? Mtu mmoja akasema: Mimi nitavinunua kwa dirham moja, Alisema mara mbili au mara tatu: Nani atajitolea zaidi ya dirham moja? Mtu mmoja akasema: Mimi nitanunua kwa dirham mbili. Alimpatia vitu hivi na kuchukua dirham mbili, na kumpatia Answaari, alisema: Nunua chakula kwa moja yake na wafikishie ukoo wako, na nunua shoka na lilete kwangu. Baadaye alilileta kwake. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliliunganisha mpini pamoja nalo kwa mikono yake na kusema: Nenda, tafuta kuni na uziuze, na nisikuone kwa wiki mbili. Mtu yule alikwenda zake na kutafuta kuni na kuuza. Alipopata dirham kumi, alikuja kwake na kumnunulia guo na baadhi yake kwa chakula. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Hili ni bora kwako (kuliko) lile, kuomba kutakuja
Pia kutokana na Sunnah, hususan ndani ya somo la Sunnah linaloitwa Suna ya Ibn Majah, tunaona kwamba Mtume wa Allaah amesema:
Kutafuta elimu ni wajibu kwa kila Muislamu.
Ujuzi wa Qur-aan na Sunnah ndio aina za elimu zilizo bora kabisa, na elimu inayonufaisha binaadamu pia ni nzuri. Qur-aan na Sunnah hazizuii usomaji wa dunia hii na ukweli Muumba Anatuhimiza kuuchunguza ulimwengu tunaoishi kwa mujibu wa aya ifuatayo kutoka kwenye Qur-aan (tafsiri):
{{Katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana, ziko hoja (za kuonyesha kuwapo Mwenyezi Mungu Mmoja), kwa wenye akili. Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa na wakilala. Na huzingatia umbo la mbingu na ardhi (pia. ‘Namna gani Mwenyezi Mungu alivyoumba.’ Wakasema) “Mola wetu! Hukuviumba hivi bure. Utukufu ni Wako. Basi Tuepushe na adhabu ya Moto.}} [3:190-191]
Chochote kilicho kizuri ndani ya makala hii kinatokana na Allaah,
na kilicho kibaya ndani yake kinatokana na sisi.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
