Muislamu Afanye Nini Anapotukanwa Mtume Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam?
SW
Mimi ninauliza swali tu jee
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Mtume, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.)
Shukrani zetu za dhati kwa maswali yako mawili. Ama kuhusu swali lako la kwanza ni kuwa yapo mengi ya kufanywa baada ya kutukanwa kwa kipenzi chetu, Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hakika yapo mengi ambao tunaweza kufanya katika
Yale tunayoweza kuyafanya ni
1. Tujue Siyrah (maisha) yake
2. Tufuate Sunnah zake kimatendo pamoja na kuwafikishia wengine hasa Waislamu, nao waige mfano wake.
3. Kuandaa makongamano kwa ajili ya kuwaelimisha wasio Waislamu na mihadhara kwa ajili ya Waislamu.
4. Kugawa vijitabu au vipeperushi kwa lugha tofauti kwa wasiokuwa Waislamu kuhusu maisha ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Mfano ni kijitabu Muhammad: The Apostle of Islam kilichoandikwa na Prof. K. S. Rama Krishna Rao na vitabu vingine vilivyoandikwa na watu wao wenyewe kuhusu Mtume kwa uadilifu.
5. Kuwa na vipindi katika idhaa za Radio na runinga.
6. Kususia bidhaa za nchi zilizofanya madhila hayo.
Ingia katika viungo vifuatavyo upate kuona hatua tuliyochukua sisi Alhidaaya alipodhalilishwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) :
Hizi hapa chini ndizo baadhi ya hatua Alhidaaya tulizofanya za kuwafahamisha Waislamu wakati alipodhalilishwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) :
Mtume Wetu صلى الله عليه وآله وسلم Amedhalilishwa, Je, Umechukua Hatua Gani Ewe Muislamu?
Mjue Mtume Wako صلى الله عليه وآله وسلم Vizuri Uzidi Kumpenda
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


