Kashata Za Njugu-Karanga
Vipimo:
Karanga Kilo
Sukari 5 vikombe
Maji 2 vikombe
Maziwa ya unga 2 vijiko vya chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Saga karanga zilizokaangwa na kumenywa mpaka zilainike kiasi.
2. Kisha changanya maji na sukari weka jikoni yachemke mpaka yanate kidogo
3. Koroga taratibu kwa moto mdogo mpaka uone imeshikana na inanata.
4. Paka mafuta treya kisha mimina na utandaze upesi upesi.
5. Acha ipoe kidogo tu kisha katakata vipande na acha ipoe kabisa.
6. Panga kwenye sahani tayari kwa kuliwa pamoja na kahawa.
Kidokezo:
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


