Du’aa Gani Ya Kuwaombea Wazazi Waliofariki Zamani?
SW
Assalamu aleikum,
Tunashukuru kwa kutufunza mengi mno ambayo tulikuwa hatuyajui
Asanteni
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukran zetu za dhati kwa swali lako kuhusu du’aa ya kumuombea marehemu mzazi au wazazi walioaga dunia. Hakika hiyo du’aa iliyopo hapo ni ile inayosomwa wakati wa kumswalia maiti katika Swalah ya jeneza. Wakati mmemaliza kuzika unaweza kumuombea mzazi wako ili Allaah Aliyetukuka Ampatie thabati ya kuweza kujibu maswali atakayoulizwa na Malaika wawili.
Ama baada ya hapo du’aa ya kuwaombea wazazi imetajwa katika Qur-aan nayo ni
Na Allaah Anajua zaidi
