Slesi Za Jibini Ya Mozzarella Na Thomu

Vipimo
Slesi Za Mikate 12
Jibini Ya Mozzarella iliyokunwa 1 kikombe
Thomu ya unga 2 vijiko vya supu
Siagi kiasi
Oregano ½ kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Paka siagi slesi za mkate.
- Nyunyizia Jibini ya mozzarella iliyokunwa (grated cheese)
- Nyunyizia thomu na oregano.
- Weka katika treya na choma katika oven kwa moto wa juu (grill)
- Zinapogeuka rangi na jibini kuyayuka toa katika oveni, panga kwenye sahani.
