Muda Wa Kurudi Katika Dini
SWALI:
Asalaam Alaikum Warahmatulhaahi Wabarakaatuhu, mimi sijambo [ Al Hamdulillaah] kama nanyi hamjambo viongozi wetu wa Dini ya kweli basi ni kheri. Naomba msaada mnijibu
3.Mtu aliyesilim kutoka kwenye Dini ya kweli kisha baada ya muda fulani akataka kurudi anaruhusiwa?
JIBU:
Shukrani zote anastahiki Allah, Mola Mlezi wa viumbe vyote. Pia shukrani ni kwa ndugu zetu kwa kaka na dada zetu wanaouliza maswali na kaka yetu huyu ambaye ameuliza haya maswali takriban tisa
3. Mtu ambaye alikuwa ni Muislamu kisha akaritadi anaweza kurudi katika Dini anapoona kuwa amefanya makosa. Na jambo hili lilitokea wakati wa Sayyidna Abu Bakar (r.a) ambapo Waarabu waliritadi na baadae wakarudi katika Dini
“Hakika walio amini, kisha wakakufuru, kisha wakaamini, kisha wakazidi ukafiri, Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaghufiria wala wa kuwaongoa njia” (4: 137).
Wa Allaahu A'alam
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


