Aibariki Manani, Tovuti Ya Alhidaaya
‘Abdallaah Bin Eifan
(Jeddah – Saudi Arabia)
(1) Narusha salaam zangu, kwa mapenzi na imani,
ziwafikie wenzangu, popote ulimwenguni,
tushike kamba ya Mungu, ya umoja na amani,
Aibariki Manani, Tovuti ya Alhidaaya.
(2) Tovuti ya Alhidaaya, Aibariki Manani,
ifike hadi ulaya, hata huko Marekani,
wazuri hata wabaya, waisome kwa makini,
Aibariki Manani, Tovuti ya Alhidaaya.
(3) Watu wananufaika, kusoma mambo ya dini,
wengi wanafaidika, makala zenye thamani,
Ndugu wanashughulika, kutuletea yakini,
Aibariki Manani, Tovuti ya Alhidaaya.
(4) Wote wanaohusika, Mungu waweke peponi,
wazidishie baraka, akhera na duniani,
waepushe na mashaka, wawe na matumaini,
Aibariki Manani, Tovuti ya Alhidaaya.
(5) Sahalisha kazi yao, gumu lifanye laini,
Hifadhi thawabu zao, katika yao mizani,
Waweke kwenye makao, makao ya wahisani,
Aibariki Manani, Tovuti ya Alhidaaya.
(6) Nchi zimeharibika, ametawala shetani,
tabia zimechafuka, kila pembe ardhini,
umeshavuka mipaka, ufisadi mitaani,
Aibariki Manani, Tovuti ya Alhidaaya.
(7) Watu wanakunywa pombe, na wanapenda kuzini,
wengine humeza chembe, na unga wa heroini,
wengine kwenye vipembe, wengine mabarazani,
Aibariki Manani, Tovuti ya Alhidaaya.
(8) Tumuombe Subhana, Aondoshe kisirani,
Awaongoze vijana, pamoja na wana-ndani,
si usiku si mchana, dua ziwe mdomoni,
Aibariki Manani, Tovuti ya Alhidaaya.
(9) Tuepuke na ghadhabu, Ghadhabu za Rahmani,
tuepuke na adhabu, ya moto na kaburini,
tuwawekee adabu, wazazi na majirani,
Aibariki Manani, Tovuti ya Alhidaaya.
(10) Hapa ndio kaditama, kalamu naweka chini,
dunia tutaihama, hapa ndio mtihani,
hapo siku ya kiama, ataepasi ni nani?
AIBARIKI MANANI, TOVUTI YA ALHIDAAYA.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha

aslamu aleykum ndungu zangu
aslamu aleykum ndungu zangu na masheikh wa kiislamu nina furaha tele kwa siku ya leyo kwanza kabisa ninawaombeya mola swt awalipe kwa haya munayo fanya iwe kwa ajili yake tu insha,allah na pili mungu awape afya ya kuweza kuendeleya ni hiyi kazi ya daawa na pia awataqabaliye amin nina taka kuuliza swali kwanza mimi nina ishi england yaani london ninauliza kuhusu sala ya ijimaa kama mfano mtu anaduka alfi mimi na dungu yangu tuko shirika na hapa london kuna swala ya ijimaa jamaa mbili ya kwanza ni mimi nina kwenda kuswali alfu ya pili ni yeye anakwenda kuswali jee thawabu ya kuhusu munye kwenda kwa sala ya ijimaa mbele anapata thawabu ya kama umechija ngamiya jee huyo ndungu yangu ambaye ameenda kusali jamaa ya pili anayo thawabu ya hiyo ngamiya au thawabu ya sala ya ijumaa au sisi sote tunayo thawabu yoyote kuhusu hiyo sala au ngamiya au misho ya thawabu ni mayai na hivi mungu ana sema katika Quran maana yake kila moja wenu wakati wa sala ya ijimaa awache kila kitu hata kama ni biashara kwa hivyo mimi nilimwabia ndungu ni uzuri mimi na wewe tufunge hii duka tuende kusali hakuna jibu na sisi hatufungi hiyi duka kwa sababu ya faida ya duniya tu jee sasa hukmu yake ni nini ndungu au masheikh wa kiislamu ni nyinyi leyo nigependa majibu yake kwa haraka sana insh,allah? suali yangu ya pili ni kuhusu sala ya kukaha like prey setting down jee hiyi enakubalika au haekubaliki basi insh,allah nina waonbeya munyeezi mungu swt awape kila lakheri na awalide na maaduwi wote wakijin na wabinadamu na mashetani wote basi kwaherini ni mimi ngungu yenu kwa jina MAHAMUD AL-AMIN QULATENI +447970654848 munaweza kunipigiya simu wakati wowote insha,allah?
Wa 'alaykumus-salaam wa
Wa 'alaykumus-salaam wa RahmatuLLaahi wa Baraakatuh
Tunashukuru kujua kwamba unafaidika na mafunzo ya Alhidaaya na tunashukuru kwa du'aa zako.
Tunasikitika kuwa hatuwezi kukujibu hapa, kwani hapa ni mahali pa kuweko maoni pekee yanayohusu makala unayosoma hapa. Hivyo tuma swali lako kupitia maswali@alhidaaya.com na Insha Allaah utajibiwa itakapofika zamu yako.
Ndugu Zako
AL HIDAAYA
Kwako zirudi salamu, Wetu
Kwako zirudi salamu,
Wetu Shaykh Eifani,
Hakika kazi ngumu,
Umeifanya bila kisirani.
Twamuomba Mola Mlezi,
Nawe Akupatie Baraka,
Uzikute zikiwa wazi,
Kukukaribisha kwa fanaka.
Kwa sasa nakomaa,
Nami naiombea mema,
Alhidaaya duniani imepaa,
Uongofu ndani imejaa.
SHUKRAN SHEIKH
SHUKRAN SHEIKH ABDELNASSERI.
(1) Salaam zangu pokea, na zako nimepokea,
Mungu Atakujalia, na wote wa Alhidayaa,
zikisafishika nia, njia itatunyokea,
Wote nawasalimia, Abdelnaseeri pia.
(2) Salaam Abdelnasseri, pamoja na Baawaziri,
na wengine wahariri, nawaombeeni kheri,
Tovuti limenawiri, Aibariki Kahari,
Hapa nasema "kwakheri," ninafunga daftari.
Abdullah bin Eifan