Haki Hii Haki Gani Mbele Ya Allaah?
Bint Ahmadah
Mwenyezi Mungu Anatusimulia moja ya visa vilivyomo katika Qur-aan Tukufu:
"Na Mariamu mtoto wa 'Imrani aliyejihifadhi nafsi yake na Tukampulizia humo roho Yetu (inayotokana na Sisi), na akayasadikisha maneno ya Mola wake, na Vitabu Vyake; na alikuwa miongoni mwa wanyenyekevu (wakubwa)." (Suratu at-Tahrym: 12)
Je kusimama mbele ya vyombo vya habari, au kwenye mikutano ya hadhara, kwa msichana na kudai haki zinazoitwa za binaadamu kwa lengo la kutembea utupu au kujifananisha na mwanaume ndio haki aliyoipigania Bibi Mariamu?
Dada yangu, haki hiyo waitaka hali ya kuwa ni kichwa kitupu kisichomuelewa Mola Mlezi utaipata wapi? Ikiwa aya za Mungu wazigeuza unavyozitaka wewe, salama utaipata wapi? Elewa ya kwamba, hao waliotaka haki ya kweli basi walijitoa kiroho, kiimani, kisubra na kinguvu kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Pitia kurasa za Bibi Fatwimah, Mama 'Aaishah na Bibi Summayyah (Radhiya Allaahu ‘Anhunna) muone namna walivyokuwa na msimamo madhubuti wa iymaan ya Uislamu. Hawakupigania haki hizo kwa ajili ya matamanio
Waislamu hawatakiwi kushirikiana na makafiri kwenye masuala ya kuzipinda kanuni za Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala)
Lengo lao kuu si jengine ila kuwaelekeza njia nyengine Waislam wauone Uislam ni mgumu usiokwenda na wakati kabisa. Wanatufanyia hila kwa nia ya kwamba Uislam uonekane unawakandamiza wanawake kudai haki
Je wanawake tupo tayari kuwa sawa na mapunda kwa kufananishwa na kitendo hicho ambacho Mwenyezi Mungu Amekikataza? Tukiona makafiri wa kike wakisimama juu ya majukwaa na wakifanya wao wana haki ya kusema kila kitu hata
Tambuwa ya kwamba hayo si ya kuiga kwa Muislam wa kweli wa kiimani na kivitendo. Haitokuwa na maana utakaposimama mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na Uislam wa kuchovya jina tu wakati vitendo huna kitu. Haki hizi zipaniwazo sio haki tunazozitaka, bali ni mabalaa ndio tunayoyaomba yatufike kutokana na maasi hayo. Kisha tunakaa vikao na kusugua vichwa kujadiliana matatizo ya dunia. Matatizo haya yanatokana na nini
Waliopita nyuma
"Hakika Tuliwapelekea upepo mkali katika siku ya nuhsi iendeleayo (kwao mpaka leo).
Ukiwang'oa watu (katika ardhi kisha unawabwata chini, wamelala, wamekufa) kana kwamba ni magogo ya mitende iliyong'olewa.
Basi ilikuwaje adhabu Yangu na maonyo Yangu!" (Suratul-Qamar: 19-21)
Je na sisi hatuyaoni majanga yote yanayotupata? Juzi
Hatutafika pahala kwa kusimama majukwaani tukidai kuwa ndio tunatetea haki zetu wanawake. Na kwa hakika, Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Habadilishi nyoyo za watu hadi wao wenyewe wawe tayari kubadilishika.
Kama Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anavyosema:
“Allaah Habadilishi hali za watu mpaka wafanye juhudi kubadilisha yaliyo nafsini mwao” (Suratu ar-Ra'ad: 11).
Huo ndio uhuru na demokrasia Aliotuwekea Mola wetu. Tupo huru kumuasi asubuhi na mchana, lakini tuelewe khatima yetu itakuwa mbaya mno:
"Na Mwenyezi Mungu Anapowatakia watu adhabu hakuna cha kuzuia wala hawana mlinzi yoyote badala Yake (Mwenyezi Mungu)." (Suratu ar-Ra'ad: 11).
Tujitahidi kurejea kwa Mola wetu kikweli na tulete toba iliyo ya kweli na tuache yale yote Mola Mlezi Aliyoyakataza.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


