Mchuzi Wa Kuku Wa Nazi Na Mayai Ya Kuchemsha

Mchuzi Wa Kuku Wa Nazi Na Mayai Ya Kuchemsha

     

Vipimo

Kuku - 2 Lb (ratili) 

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu 

Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu 

Bizari ya pilau ya unga- ½ kijiko cha chai 

Ndimu - 1 kamua maji 

Chumvi - kiasi 

Bizari manjano - ½ kijiko cha chai 

Vitunguu maji - 1 

Nyanya - 2 

Tuwi la nazi zito - 1 ½ kikombe 

Mayai ya kuchemsha - 6 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Mchemshe kuku na thomu na tangawizi na ndimu na chumvi mpaka akauke.
  2. Saga vitunguu na nyanya kidogo tu kwa kutumia tui kidogo katika mashine  (blender).
  3. Mimina kwenye kuku pamoja na bizari zote.
  4. Acha achemke kisha tia tui lichemke mpaka liwe zito
  5. Tia mayai ya kuchemsha.
  6. Pakua kwenye bakuli tayari kuliwa na wali au mkate.

 

Share