Viazi Vyekundu Vya Masala

Viazi Vyekundu Vya Masala

      

Vipimo:

Viazi /mbatata - 10 kiasi 

Kitunguu maji kilichosagwa -  1 

Kitunguu maji(thomu/galic) iliyosagwa -  1 kijiko cha supu 

Pilipili iliyosagwa - 1 kijiko cha chai 

Rai (mustard seeds) -  1 kijiko cha supu 

Majani ya mchuzi (curry leaves)  -  7 majani  

Uwatu uliosagwa (methi) -  1 kijiko cha chai 

Nyanya kopo - 5 vijiko vya supu 

Ndimu - 3 vijiko vya supu 

Mafuta -  ¼ kikombe 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Chemsha viazi kiasi viwive lakini  visivurugike
  2. Menya, katakata vipande weka kando.
  3. Tia mafuta katika sufuria, yakishika moto tia rai, zikaange kwa muda wa dakika moja hadi zigeuke rangi kidogo.
  4. Tia majani ya mchuzi, uwatu, thomu, kitunguu maji, pilipili  kaanga kidogo tena.
  5. Tia nyanya kopo endelea kukaanga kidogo kisha tia chumvi, ndimu na maji kiasi kidogo ili kufanya rojo kiasi.
  6. Mimina viazi, changanya, pakua katika sahani.

 

Share