Akiota Ndoto Ya Jimai, Mchana Wa Ramadhaan, Afanye Ghuslu? Je, Aendelea Na Swawm Au Inabatilika?
SWALI:
Assalamu aleikum warahmatullahi wabarakatuh. Swali langu ni kuwa nimelala mchana wa ramadhan nikaota ndoto ya utu uzima, nikaamka na kuona majimaji kwa nguo yangu. Je nitaoga josho la janaba ama nitaendelea na saum yangu.
Jazakallahu kheir.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Asli katika mas-ala ni kuwa swawm ya mtu mume au mke haibatiliki kama ataamka wakati wa alfajiri na janaba iwe janaba kwa sababu ya kulala na ahli yake au kwa kutoa
“Kwa hakika Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wa’ala Aalihi Wasallam alikuwa inamdiriki al-fajr hali ya kuwa na janaba kutokana ahli zake, kisha hukoga na kufunga” lmepokelewa na Bukhaar, Kitabi cha Swawm, mlango mwenye kufunga na kuaamka na janaba.
Hivyo basi hukumu ni kuwa swawm haibatilika bali ipo na inaendelea kwa kila atae lala mchana na kuota ndoto ya utu uzima, awe mwanamume au mwanamke.
Kitacho kulazimu ni kukoga josho na kuendelea na swawm yako na huna kulipa wala fidia kwani huna kosa lo lote.
FAIDA: Kuyatoa manii –maji ya uzazi- kwa makusudi iwe kwa mkono au kwa kuchezewa na Mkeo au kwa kutazama kwa matamanio mpaka yakatoka au njia yoyote ile itayo kuwa na shahwah, funga inabatilika na itamlazimu muhusika kuilipa siku hiyo. Ama yakiwa yametoka kwa kutazama -bila kukusudia- basi haiharibu Swawm yake.
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


