Uji Wa Kunde

Vipimo
Kunde Kavu 2 Vikombe
Tui 1 Kikombe
Sukari 1 Kikombe
Maji 7 Vikombe
Garam masala ½ Kijiko cha chai
Hiliki Kiasi
Karafuu 3-4 Chembe
Pilipili manga ½ Kijiko cha chai
Chumvi Chembe kidogo
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Chemsha kunde kavu bila yakuroweka kwa maji vikombe 4 na sukari kikombe kimoja kwa moto kiasi mpaka ziwive
- Kisha mimina vitu vyote vilivyobakia pamoja na maji vikombe 3 vilivyobaki na acha ichemke taratibu mpaka
maji yapunguke uji uwe mzito..
- Epua mimina kwenye bakuli ukiwa tayari
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
