Kaimati (Aina Ya 3)

Vipimo
Unga 2 vikombe vya chai
Hamira 1 ½ cha chai
Samli 1 kijiko cha chai
Maji 1 ½ kikombe cha chai (kiasi)
Mafuta ya kukaangia kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Changanya unga Hamira, Samli, maji, kisha vuruga kulainisha unga hadi uwe hauna madonge na mwepesi kiasi.
- Funika unga uumuke. Ukiuumuka (ukifura) choma kaimati katika mafuta ya moto.
- Ziepue na zichuje mafuta.
- Weka kaimati katika bakuli au sahani kisha mwagia *Shira zikiwa tayari.
Shira:
Sukari 3 vikombe
Maji 1 kikombe
Hiliki ¼ kijiko cha chai
Arki (rose flavour) 3-4 matone
Namna Ya Kutayarisha Shira
- Tia sukari na maji katika kisufuria kidogo, acha kwenye moto ichemke pole pole hadi iwe nzito ya kunata.
- Tia hiliki na arki ikiwa tayari kumwagiwa juu ya kaimati, huku unavichanganya na huku shira ikipowa na kugeuka kuwa sukari kavu.
Kidokezo:
Shira ya Kaimati hizi iwe nzito ili unapochanganya na kaimati igeuke kuwa
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
