Kuna Du’aa Ya Kunuia Kwa Ajili Ya ‘Iyd
SWALI:
asalamu aleikum ndugu zetu al hidaaya tunashukuru
basi ndugu naomba mutufune jinsi ya kunuwia idul fitri basi munielze dua yake ndugu zangu kwa haya machche shukran
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Hatukupata mafunzo yoyote yaliyo Swahiyh kuhusu kutia nia kwa ajili ya Sikukuu ya 'Iydul-Fitwr wala 'Iydul-adhwhaa na wala hakuna du'aa khaswa iliyothibiti katika mafunzo ya dini yetu.
Ikiwa umekusudia kutia nia kwa ajili ya Swalah ya 'Iyd basi
Bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Chapisha
- Kutuma Kwa Email
