Gulab Jamun Nyeupe (Pakistani)

Gulab Jamun Nyeupe (Pakistani)

 

Vipimo

Maziwa fresh - 2 L (lita)

Siki - ¼  Mug

Maji - ¼  Mug

Sukari - 1 ½ kijiko cha chai

Unga wa ngano - 1 kijiko cha chai

Unga wa semolina - 1 ½ kijiko cha supu

Baking powder - ¼ kijiko cha chai

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Chemsha maziwa mpaka yachemke.
  2. Changanya siki na maji umimine kwenye yale maziwa yaliyochemka, maziwa yatakatika yatafanya kama mtindi halafu epua motoni
  3. Chuja kwa chujio maji yote yatoke na wacha mpaka ipoe ukamue maji yote.
  4. Mimina kwenye bakuli changanya na unga wa ngano na unga wa semolina na baking powder kisha ufanye viduara vidogo dogo kama shepu ya mayai.

 

Shiyra  (Ya Kumimina Juu Yake)

Sukari - 3 vikombe

maji - 2  vikombe

 

Chemsha motoni aacha mpaka ichemke  na iwe nzito kiasi, kisha mimina vile vidonge kwenye shiyra, chemsha kwa moto mkubwa kwa muda wa dakika 20 na moto mdogo kwa dakika 20 epua tayari kwa kuliwa  .

 

 

Share