Du’aa Gani Asome Ili Apate Mume Wa Kheri?
SW
Assalam Aleikum,
Kwanza nawapongeza
Lakini naomba niwaulize swali moja linalonisumbua siku nyingi
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Du’aa ya kupata mume.
Hakika ni kuwa hatujapata kuona wala kusikia Du’aa
Tufahamu kuwa Allaah Aliyetukuka Hakutuachia kitu chochote isipokuwa Ametuelezea kama Alivyosema katika Qur-aan:
“Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote. Kisha kwa Mola wao Mlezi watakusanywa” (6: 38).
Swali linaweza kuja kwa nini basi hakuna Du’aa ya kupata mume wa kheri? Jibu kwa swali hili ni kuwa Allaah Aliyetukuka Ametuambia:
“Niombenei Nami nitawajibu”.
Na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) naye ametuelezea nyakati ambayo Du’aa inakuwa ni yenye kukubaliwa kwa urahisi kabisa. Hivyo, inabidi ujitume ili kufikia
1. Baina ya Adhaana na Iqaamah.
2. Thuluthi ya mwisho ya usiku ambamo utainuka uswali Tahajjud, na humo uombe.
3. Ukiwa katika sijdah ndani ya Swalah.
4. Siku ya Ijumaa baina ya Khutbah mbili.
5. Baada ya Alasiri siku ya Ijumaa na kabla kuchwa jua.
6. Uwe ni mwenye kula, kunywa, kuvaa vya halali na uwe ni mwenye kumridhisha Allaah Aliyetukuka.
7. Wakati unapokuwa safarini.
8. Wakati unapokuwa umefunga, funga ya Faradhi (Ramadhaan) au ya Sunnah. Hivyo, jaribu kujikurubisha kwa Allaah kwa kufunga Jumatatu na Alkhamiys na ndani yake nyenyekea kwa Allaah.
9. Kabla hujatoa Salaam ndani ya Swalah.
Fanya bidii umuombe Allaah, naye Atakupa mwenye kheri na mswalihina InshaAllaah wala usife moyo katika
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


