Khalyat An-Nahl - Mzinga Wa Nyuki -2

Vipimo
Unga 4 Magi (vikombe vya chai)
Maziwa ya maji 1 ½ au 2 Magi
Sukari 1 Kijiko cha supu
Mafuta Robo Magi
Hamira 1 Kijiko cha supu
Chumvi robo kijiko cha chai
Cheese ya Cream 1 Kikopo au Pakti
Baking powder 1 Kikombe cha chai
Shira
Sukari Vikombe 2
Maji Kikombe 1 ½
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Changanya vitu vyote hivyo isipokuwa cream cheese.
2. Kanda kidogo tu kulainisha unga uwe mlaini
3. Pakaza siagi katika sinia ya round utakayopikia
4. Fanya viduara vidogo vidogo na tia ndani yake cheese ya cream kwa kutumia kijiko cha chai, na vifunge viduwara vizuri na kuvipanga katika sinia bila ya kuwacha nafasi.
5. Iwache iumike kisha paka maziwa juu yake kwa brashi kabla ya kuchoma ili kufanya ing’are.
6. Ipikie katika oven moto wa chini kwanza katika 350˚C, kwa muda wa baina dakika 20 na 25 . Kisha washa moto wa juu kidogo tu uwive kwa juu.
7. Toa katika oven na mwagia shira
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


