Slesi Za Chokoleti Na Karameli

Slesi Za Chokoleti Na Karameli

  

 

Vipimo

Unga - 1 Magi (vikombe vya chai)

Sukari ya browni -   ½ Magi              

Siagi iliyoyayushwa   - 125 g

Nazi iliyokunwa - ½ Magi              

 

Mjazo wa karameli  (Caramel filling)                                                   

 

Syrup - 1/3 kikombe cha chai

Siagi iliyoyayushwa -  125 g 

Maziwa matamu ya mgando - 2 vikopo (condensed milk) 

 

Mjazo wa chokoleti (Chocolate filling)

 

Chokoleti  - 185 g (dark chocolate) 

Mafuta  - 3 Vijiko vya chai 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Changanya unga, sukari, siagi na nazi iliyokunwa kwenye bakuli mpaka unga ushikamane.
  2. Paka mafuta treya ya kuchomea kisha utandaze kwenye treya ya 20cm kwa 30 cm au (8 in kwa 12 in) unaweza kuweka karatasi ya kuchomea chini ukipenda.
  3. Choma kwenye moto 325˚C kwa muda wa dakika 15 mpaka 18 au mpaka ibadilike kuwa rangi ya browni.
  4. Kwenye sufuria ndogo  tia syrup siagi na maziwa matamu ya mgando na changanya kwa moto mdogo mpaka uwe mzito kasha mimina juu ya keki uliyochoma na choma tena kwa muda wa dakika 20 mpaka karameli iwe rangi ya dhahabu.
  5. Kwenye sufuria ndogo nyingine tia vipande vya chokoleti na mafuta na ukoroge kwa moto mdogo mpaka iyayuke kisha wacha ipoe kidogo mimina juu ya mjazo wa karameli kisha weka kwenye friji mpaka ishikamane.
  6. Kata vipande weka kwenye sahani tiyari kwa kuliwa

 

 

 

Share