Je, Inanyanyuliwa Mikono Katika Kila Takbiyrah Ya Ziada Kwenye Swalaah Ya 'Iyd?

Je, Inanyanyuliwa Mikono Katika Kila Takbiyrah Ya Ziada Kwenye Swalah Ya 'Iyd?

 www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Assalam Aleyqum,
 
Je baada ya kufunga swala  katika swala IDD unapo piga TAKBIRA je unainua mikono kama unafunga swala au unapiga takbira wakati mikono ikiwa umeifunga kifuani kama kawaida ?

 

 

 

JIBU:

 

 AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Suala la kunyanyua mikono kwenye Swalah ya 'Iyd katika Takbira za ziada halijathabiti kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) bali limefanywa na Maswahaba kama Ibn 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhuma). Na ndio Maulamaa wakasema kutokunyanyua mikono ndio sahihi zaidi kwa sababu Mtume hakufanya hivyo. Lakini pia wamesema ikiwa mtu atanyanyua mikono hakuna tatizo kwani baadhi ya Maswahaba walifanya hivyo.
 
Kwa hiyo, utakapokuwa unaswali Swalah ya 'Iyd, utanyanyua mikono yako katika kufunga Swalah wakati wa Takbiyratul Ihraam, kisha baada ya hapo utaiacha mikono yako kifuani bila kuinyanyua wakati unapopiga hizo Takbiyrah saba za ziada katika rakaa ya kwanza na zile tano katika rakaa ya pili.
 
Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share