Taratibu Za Wudhuu
SWALI:
Ukisahau kuosha viganja vya mikono na umeosha uso mara moja, je unaweza kurudi kwenye mikono bila ya kuanza udhu upya?
JIBU
Ukisahau ukatia wudhuu kiungo kingine kabla ya kile kinachotakiwa ni bora kuanza wudhuu upya kwani ni katika sharti za wudhuu kufanya kwa mpangilio wake kuanza viganja vya mikono, kusukutua na pua, uso, mikono, kichwa na masikio na miguu.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


