Damu Ya Hedhi Inayoendelea Kwa Muda Mrefu
SWALI:
asalam alaikum warahma tullahi wabarakatum, mie nina suala linanitatiza , ukweli mimi nimejaribu kuweka luppu na madaktari wamenambia inachukua muda wa miezi 3 nitakuwa nableeding na kweli mpaka leo karibu miezi 2 na nusu naendelea kubleeding sasa suala langu hili, kuna watu wamenambia naweza kufunga na kusali nijisafishe tu haya ni maradhi sio hedhi, na kuna wengine wananambia kuwa siwezi kusali lkn kufunga naweza sasa nimeshindwa kufahamu lkn mimi nafunga kutoka sijajua ukweli wenyewe, na pia najiuliza nafsi yangu kuwa nafunga bila ya kusali, nakuombeni munisaidie kwa suala hili linanitatiza sana .inshallah nategemea mtanijibu kwa ufasaha kwa uwezo wake allah (a.w) inshallah nategemea jibu lenu haraka
JIBU:
Shukrani kwa Allah kwa kutupatia fursa hii kubwa.
Kwa hakika hii yako ni damu ambayo si ya kawaida na huwa ni ugonjwa kwa hivyo kisheria huitwa Istihadhwa. Na hukumu yake ni kuwa iwapo mwanamke alikuwa kabla ya kuwa na damu hiyo ya ugonjwa, ni mzoefu, na anazijua siku zake za ada yake katika kila mwezi. Katika siku hizo hatafunga wala hataswali. Baada ya kumalizika siku hizo ataoga na ataswali na atafunga na ataingiliwa ikiwa ameolewa.
Na akiwa amesahau muda wake au idadi ya siku zake, basi akiweza kupambanua damu, ikawa inatoka mara nyeusi, mara nyekundu, akiona rangi ya kawaida haipo tena na inatoka rangi nyengine ataoga na kutekeleza ‘Ibadah zake zote. Ghalibu ada inakuwa kwa siku 6 au 7 kishaa ataoga na kuswali pamoja na kufunga.
Na mwenye damu ya ugonjwa katika siku za kuwa katika hali hiyo atatawadha baada ya kuoga na ataweka kitamnbara au nguo au pamper katika sehemu yake ya siri na ataswali ijapokuwa damu inamiminika kwa nguvu. Ataunganisha Swalah ya Adhuhuri na Alasiri kwa kuichelewesha Adhuhuri na kuiswali mapema Alasiri na hivyo hivyo Magharibi na Ishaa kwa kuichelewesha Magharibi. Na hii ndio njia aliyoipenda Mtume (s.a.w.) {Abu Dawud, at-Tirmidhy na Ahmad kutoka kwa Himnah bint Jahsh [r.a.]}.
Hivyo, wakati mwanamke anapokuwa ana shida ya kutokwa na damu nyingi anatakiwa aswali na afunge
Na Allah Anajua zaidi.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


