Skip navigation.
Home kabah

Viazi Vya Kukaanga Na Sosi Ya Nyanya

 

 

 

 

 

Vipimo

 

 

Viazi                                     5 vya kiasi

 

Bizari ya manjano                  ½ kijiko cha chai

 

Meti ya unga                          ½ kijiko cha chai

 

Mafuta                                     2 kijiko cha supu

 

Limro (majani ya kihindi)           6 majani

 

Nyanya                                    1

 

Pilipili mbichi                             3

 

Ndimu                                     1

 

Chumvi                                   kiasi

 

kidonge cha supu                  ½

 

Nyanya kopo au paprika        ½ kijiko chai

 

Maji                                      ½ kikombe

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

 

 

1       Katakata viazi virefu virefu kama uonavyo kwenye picha.

 

2        Tiia mafuta kwenye sufuria, bizari ya manjano, meti, chumvi, kidonge cha supu na maji kisha funika na acha moto mdogo mpaka viive bila kukoroga.

 

3      Tia nyanya, pilipili mbichi, nyanya ya kopo au paprika na ndimu, funika moto mdogo na huku unakoroga. kisha utaonja na itakuwa tayari kwa kuliwa.

 

 

A.aleykum,shukran alhidaya

A.aleykum,shukran alhidaya kwa recipes.Nauliza viazi unaeka kwenye step 2 ama 3?

Wa'alaykumusalaam

Wa'alaykumusalaam Warahmatullahi Wabarakatuh

Ndugu mpenzi, tunatumai kuwa unafaidika pia na chakula cha moyo. Kuhusu swali lako, viazi vinakaangwa pale unapotia mafuta pamoja na vitu vya step 2.

Ndugu Zako

Alhidayaa.

Rudi Juu