Laylatul-Qadr: Siruhusiki Kwenda Masjid, Inafaa Kufanya Adhkaar Nyumbani Kumi La Mwisho?

 

 

Laylatul-Qadr

Siruhusiki Kwenda Masjid, Inafaa Kufanya Adhkaar Nyumbani Kumi La Mwisho?

 Alhidaaya.com

 

 

 

 

SWALI:

 

Mimi huwa nakaa macho na kusoma kuran na kuswali tahjud, kuomba dua, kumtaja Allah kwa adkhaar katita kumi la mwisho wa mwezi wa ramadhani nikiwa nyumbani je ninafanya makosa? Nimesoma kwenye alhidaaya kuwa itikafu haikaliwi nyumbani je nifanye nini nami nataka kupata dhawabu zake na msikiti wetu hawaruhusiwi wanawake kukesha.

 

 

 

JIBU:

 

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho. 

 

 

Hakika ni kuwa adhkaar unaweza kuleta mahali popote na wakati wowote ule isipokuwa chooni lakini I‘tikaaf haifanywi isipokuwa katika Msikiti. Jambo linalotakiwa kutoka kwenu ni kuweza kuzungumza na Imaam kuhusu kuruhusiwa kwa wanawake kufanya I’tikaaf kama walivyofanya Swahaba wa kike (Radhwiya Allaahu ‘anhunna) wakati wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakiwemo wakeze.

 

Ikiwa wameshindwa kuwapa ruhusa nyinyi hamna haja kuhuzunika kwani ‘amali zote hutazamwa na kutegemea Niyyah. Niyyah yako au yenu ikiwa nzuri basi mtapata thawabu kamili japokuwa hamkukaa I’tikaaf hiyo ndani ya Msikiti. Hata hivyo, nyumbani huko unaweza kuleta adhkaar, kusoma Qur-aan na kufanya mengineo ya kukupatia thawabu nyingi mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

Bonyeza viungo vifutavyo upate maelezo zaidi:

 

Fataawaa: Qiyaam Al-Layl: Tarawiyh Tahajjud Witr

 

Fataawaa: Kujuzu Au Kubatilika Swawm, Kulipa Na Kafara: Hedhi, Mja Mzito, Kunyonyesha, Nifaas

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share