Kuweka Du’aa, Qur-aan Au Adhaan Kuwa Mlio Wa Simu

SWALI LA KWANZA:

 

asalam alaikum narudia kutuma ili swali mwanzo sikujibiwa.swali ni kwamba inafaa kutumia quraan kama mlio wa simu? kuweka liowa mpigaji au miito ya simu kutumia sura yeyote au adhana & dua najua unaweza kutumia qaswida. nitashukuru sana kila la kheri katika kuendeleza mtandao wa alhidaaya.

 

SWALI LA PILI:

 

 

 

Assalam alaikum, swali langu ni kwamba mtu anaposeti mlio wa simu msomaji wa quram ni sahihi maana sio wote tunaepokea na na kupiga ni waisilam, pia simu inapoita kwa aya ya quran jina la mwenyezi mungu hata alijaisha ikapokelewa sijui inafaa au haifai au tanafanya tukitu hatuna hakika nacho inshallah nitakua nimeeleweka,


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuweka Aayah ya Qur-aan au Adhaana kuwa mlio wa simu. tunasikitika kuwa jibu kwa swali hili hukupata lakini tulilijibu kitambo sana. Hata hivyo jawabu lakenikama lifuatavyo:

 

Hakika ni kuwa Muislamu hafai kuweka mlio wa simu kuwa ni Aayah au surah ya Qur-aan kwani Qur-aan haikuteremshwa kwa lengo hilo. Allaah Aliyetukuka Anasema:

Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi” (al-Baqarah [2]: 185).

 

Na kisha Qur-aan haifai kusomwa katika sehemu fulani mojawapo ikiwa ni chooni. Mfano umeingia chooni na ikaanza kulia utafanya nini? Itabidi uizime lakini hasara tayari itakuwa imepatikana. Pia ikianza kuita au kulia nawe uipokee, hata kabla ya kumalizika Aayah itakuwa ni utovu wa adabu.

 

Ama sauti ya Qur-aan kusikika na asiye Muislamu haina shida kabisa bali ndio lengo lake, Kitabu hicho kitukufu. Ikiwa asiye Muislamu anataka kujua kuhusu Uislamu licha ya kusikiliza hata kuisoma kwa kupatiwa tafsiri kwa lugha anayoielewa ndio bora na lengo.

 

Kwa hiyo, jambo hilo halina shida kabisa katika shari’ah.

 

Bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:

 

Kuweka Milio Ya Miziki Kwenye Simu Za Mkononi Au Qur-aan Inayosomwa Au Adhaana

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share