Kuku Wa Kuchoma (Grilled) Wa Sosi Ya Haradali Na Slesi Za Viazi

Kuku Wa Kuchoma (Grilled) Wa Sosi Ya Haradali Na Slesi Za Viazi

Vipimo

Kuku -  5-6 Lb Mapaja na miguu

Kitunguu saumu/thomu iliyosagwa - 1 kijiko cha supu

Tangawizi ilosagwa - 1 kijiko cha supu

Mtindi (Yoghurt) - 1 kijiko cha supu

Sosi ya haradali (mustard) - 2 vijiko vya supu   

Sosi ya pilipili nyekundu -  2 vijiko vya supu

Ndimu - 2 vijiko vya supu

Chumvi - Kiasi

Jira (bizari ya pilau ya unga/cummin) - 1    kijiko cha chai

Gilgilani ya unga (coriander powder)  - 1  kijiko cha chai

Mdalasini wa unga - ½ kijiko cha chai

Pilipili manga - ½  kijiko cha chai                 

Viazi -  4-5 vikubwa

Unga wa ngano - 2 vijiko vya supu                                 

Mafuta ya kukaangia viazi - kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Safisha vipande vyako vya kuku kisha vichuje maji.
  2. Changaya viungo vyote kwenye bakuli   
  3. Tia vipande vya kuku uchanganye na masala hayo kisha roweka kwa muda wa saa au zaidi. Kila akiroweka zaidi huzidi kukolea viungo.
  4. Menya viazi na vikate slesi za duara weka kando.
  5. Panga kuku katika treya na mchome katika oveni moto wa juu (grill) huku unageuza hadi kuku akaribie kuiva. Unaweza kumchoma  kwenye jiko la mkaa vilevile. Akishaiva epua na panga kuku katika sahani.
  6. Tia viazi katika bakuli ulorowekea kuku litakuwa limebakisha sosi ya kuku uchanganye viaizi vizuri.
  7. Nyunyizia unga wa ngano katika bakuli la viazi, kisha vikaange kwenye mafuta mpaka viive, vitoe uchuje mafuta.   
  8. Vipange katika sahani pamoja na kuku vikiwa tayari

 

Share