Wametofautiana Wakajenga Msikiti Mwengine Kando Yake Na Yote Inaswalisha Ijumaa, Je Msikiti Upi Unaopasa Kuswaliwa?
SWALI:
Namshukuru
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kujenga Msikiti mwingine kwa sababu ya kutofautiana. Hata hivyo, inaonyesha kuwa swali lako halikukamilika ili kuweza kukusaidia kwa njia nzuri. Umesema tu Waislamu wametofautiana, kivipi, kwa misingi gani, na mengineyo. Kwa hiyo, tujaribu kukujibu kwa ujumla ili upate nadharia ya sawa na hapo huenda swali lako likajibiwa.
Tofauti baina ya Waislamu zitaendelea kuwepo mbali na kuwa Allaah Aliyetukuka ni Muweza wa kuwafanya kitu kimoja. Allaah Aliyetukuka Anatulezea kuwa maadamu Waislamu ni wanadamu basi wataendelea kutofautiana: “Na Mola wako Mlezi Angelipenda Angewafanya watu wote wakawa ummah mmoja. Lakini hawaachi kukhitalifiana” (Huud [11]: 118). Na kwa ajili hiyo, Waislamu kama wanadamu huenda wakagombana, lakini wanapofikia hadi hiyo ni lazima kupatikane ufumbuzi wa tatizo lenyewe. Allaah Aliyetukuka Anasema: “Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Allaah ili mrehemewe” (al-Hujuraat [49]: 10). Waislamu wakitofautiana hawafai kuacha tatizo
Kujengwa Msikiti mpya inahitajika katika Dini ili iwe sahali kwa kila Muislamu kupata jamaa lakini kuanzishwa huko Msikiti mpya kusiwe kwa malengo ya maslahi, kuwatumikia maadui, ukabila na urangi au tofauti ndogo ambazo si za msingi. Hata hivyo, ikiwa tofauti ni katika ‘Aqiydah kumaanisha kuwa walioanzisha Msikiti mpya ni kutoroka ‘Aqiydah mbaya zenye kumtoa mtu katika Uislamu katika msikiti wa zamani au mabid’ah mengi basi kuanzishwa Msikiti huo kutakuwa hakuna tatizo kisheria bali litakuwa ni jambo linalohitajika. Ama ikiwa walionzisha msikiti mpya ni kuhuisha ‘Aqiydah mbaya na bid’ah ambazo ni upotevu katika Dini Msikiti huo utakuwa ni wa kuleta madhara na unahitajiwa ususiwe na Waumini.
Katika mji mmoja kunaweza kuwa na majumaa hata zaidi ya mawili au kumi kutegemea wakaazi wenyewe na idadi
Ama kuhusu masharti ya Ijumaa ni
1. Kuwe na jamaa, na jamaa ni kuanzia watu wawili, yaani Imaam na mtu mmoja
2. Jamaa iwe ni ya watu walio huru, wanaume, wakaazi na wenye akili timamu.
Yakipatakana masharti hayo tayari Msikiti huo unaweza kuswali Swalaah ya Ijumaa. Mbali na kuwa tumetangulia kusema ikiwa Msikiti mmoja unawatosha wakaazi wa mji basi hakuna haja ya kuwa na juma la pili.
Na Allaah Anajua zaidi.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
