Hukmu Ya Kufanya Dhikr Kwa Pamoja Msikitini

SWALI:

 

Assalam aleykum.. kwanza napenda to pongezi kwa kuanzisha  website hii, inatusaidia sana hasa kwa sie tulio ughaibuni,Mwenyezi Mungu (Subhanah Wa taalah) awajaze majazo mema.

Swali langu ni hili... nilipokua nyumbani (tanzania) chuo chetu kilikua cha dhikri nadhani nikisema hivo utakua umenielewa... NACHOTAKA KUJUA SASA JE DHIKRI NI HALAL AU LA? NA JE KAMA NI HALAL AU HARAM KUNA USHAHIDI WOWOTE?  A.aleykum warahma tullah wabarakat..

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Hakika dhikr (utajo wa Allaah) ni jambo ambalo limehimizwa sana na Allaah Aliyetukuka na Mtume wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Hata hivyo, njia ya kuifanya ndio inafanya iwe halali au haramu. Allaah Aliyetukuka Anasema kuhusu kumdhukuru:

Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Allaah kwa anayemtaraji Allaah na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Allaah sana” [Al-Ahzaab [33]: 21].

Na Anasema pia:

Na wanaomdhukuru Allaah kwa wingi wanaume na wanawake, Allaah Amewaandalia msamaha na ujira mkubwa” [Al-Ahzaab [33]: 35].

 

Sasa jinsi yakutekeleza dhikr ndio muhimu na kuhusu hilo tumepata maelekezo kutoka kwa Qur-aan yanayosema:

Na mkumbuke Mola wako nafsini kwako kwa unyenyekevu na khofu, na bila ya kupiga kelele kwa kauli, asubuhi na jioni. Wala usiwe miongoni wa walioghafilika” [Al-A’raaf [7]: 205].

 

Kwa minajili hiyo, dhikr za watu kukusanyikana na kukohoa hazipo katika shari’ah yetu na hiyo inakuwa haramu.

 

Ama mtu kukaa Msikitini au nyumbani kwake au sehemu yoyote ile na kuanza kumtaja Allaah Aliyetukuka kama alivyotufundisha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni jambo zuri linalopendekezwa sana.

 

Na watu kupoteza wakati kwa kuwaingiza watoto wao au vijana wao kwenye vyuo kama hivyo vya kudhikiri kwa kupiga kelele na kukohoa na maneno ya ‘Huw’ ‘Huw’ au kufundishwa kupiga twari (dufu) ni mambo yasiyo na manufaa kwa Dini yao wala kuwaongezea Iymaan, isitoshe ni mambo yenye kuwapotezea wakati wao na miaka ambayo wangejifunza mambo muhimu kama Tawhiyd, ‘Aqiydah, Qur-aan, Hadiyth, Fiqh ambayo ndio mambo ya msingi Muislamu kuyafahamu na yenye kuweza kumsaidia kuongeza Iymaan yake na kumpeleka Peponi.

 

Kwa hiyo, ni muhimu sana wazazi na watu kuchagua vyuo vya kuaminika vya watu wa Ahlus Sunnah wal Jama’ah wenye kufundisha Uislamu kama ulivyokuwa ukifahamika na Salafus Swaalih (Wema waliotangulia; Maswahaba, Matabiina na waliowafuata Matabiina).

 

Kwa maelezo na manufaa zaidi, bonyeza viungo vifuatavyo:

 

Kusoma Uradi Kwa Pamoja Kila Mwezi Kwa Kukusanyika Inafaa?

 

Kumuombea Du'aa Mgonjwa Kwa Mkusanyiko Inafaa?

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share