Saladi Ya Matango, Capsicum, Nyanya Dressing Ya Parsley

Saladi Ya Matango, Capsicum, Nyanya Dressing Ya Parsley

 

Vipimo

 

Saladi  ya uwa (lettuce wrap/iceberg) - 1

Matango - 3

Pilipili boga (capsicum) - 2

Nyanya/tungule - 4

 

Namna Ya Kutayarisha

  1. Chambua saladi, osha kisha chuja maji, kisha katakata na weka katikati ya sahani ya saladi.
  2. Katakata nyanya/tungule zungushia pembeni yake.
  3. Katakata tango zungushi pembeni ya nyanya/tungule.
  4. Katakata pilipili boga (capsicum) weka katikati ya saladi.

Vipimo vya Sosi Ya Saladi ya Parsely (Parsely salad dressing)

 

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 3  chembe

Parsley (aina ya kotmiri) kavu - ¼ kikombe

Pilipili manga au nyekundu ya unga - 1 kijiko cha chai

Mafuta ya zaytuni (olive oil) - ¼ kikombe

Siki au ndimu - 3 vijiko vya supu

Chumvi - kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha

  1. Chuna (grate) au saga kitunguu thomu, kisha weka katika kibakuli.
  2. Changanya na viungo vilobakia.
  3. Wakati wa kula, mwagia juu ya saladi.
  4. Kidokezo:
  5. Ukikosa parsley kavu, tumia freshi.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share