Mtoto Atumie Njia Zipi Za Kumnasihi Mama Anapokosea Bila Kusababisha Kutokuelewana

SWALI:

 

ikiwa mama ana makosa juu ya mtoto na mtoto afanye nini kunjulisha mama eli mama afahamu bila kutoelewena  na mamake  na mtoto asifanye chuki na mamake.


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu jinsi ya mtoto kumnasihi mama yake.

Nasaha na kuamrisha mema na kukataza maovu ni muhimu ifanywe kwa njia nzuri, kwa hekima na mawaidha mazuri. Na haya yatakiwa yafanywe kwa yeyote yule sio mama tu kwani Allaah Aliyetukuka Anatuelezea:

Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mema” (an-Nahl [16]: 125).

 

Kwa minajili hili mtoto anaweza kutumia njia nyingi za upole na nzuri ili kurekebisha makosa hayo. Njia hizo ni kama:

 

1.     Kumpatia mama vitabu kwa lugha anayoielewa kama vile Qur-aan na tafsiri yake, Muislamu anavyopaswa kuwa, Iymaan na maelezo yake, Siyrah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Visa vya Manabii na Maswahaba. Baada ya hapo unaweza kuja katika tatizo alilo nalo mama.

 

2.     Kumpatia kanda za kusikiliza, video, VCD, DVD za mawaidha ya Kiislamu.

 

3.     Kumhimiza kuhudhuria mihadhara, darsa na khutbah za Ijumaa.

 

4.     Kumshirikisha na vikundi vya kinamama wenye Msimamo wa Sunnah.

 

5.     Kutumia watu wake na wako wa karibu katika kurekebisha hali hiyo.

 

6.     Na njia nyenginezo ambazo unaziona ni munasibu kutegemea na mazingira yenu.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share