Skip navigation.
Home kabah

Nini Fidya Ya Kutokufunga Ramadhaan Zilizopita?

SWALI:

Assalamu allaikum wa rahmatullulahi

Nina sikitiko sana, nimepitwa na ramadhani mbili mufililizo bila kufunga kwa juu nimekuwa na mimba ya watoto wangu( two following years I  had two children)je sikufanya fidiya,awo kulipa hizo siku zote 60.Nimewawuliza mashehe, nimejibiwa kwamba kwaju nimekuwa na mimba si mana kulipa hizo siku hawo kulipa fidhiya.Je ni kweli hawo?

Nasikitika sana kwa hili swali.

RAMAZANI  KARIMU KWA WAISILAMU WOTE

ASSALAU ALAIKUM

 


  

 

JIBU:

Sifa zote njema anastahiki Allah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum)  na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

Shukran kwa swali la dada yetu ambalo ni muhimu katika utendaji kazi na utekelezaji wa ‘Ibadah katika Dini yetu tukufu. Tunamuomba Mola wetu Mlezi ampatie thabati dada yetu na hima katika Dini pamoja nasi sote Waislamu katika ulimwengu.

Jambo ambalo ni maarufu ni kuwa yeyote anayekula katika mwezi wa Ramadhani kwa sababu inayokubalika kisheria kwa mfano safari, kunyonyesha na kubeba mimba (ikiwa atahofia afya yake au ya mtoto wake), ugonjwa, wanawake katika damu ya mwezi au baada ya kuzaa, na kadhalika ni wajibu kwake kulipa siku alizokula. Hii ni kwa kauli ya Allah (Subhaanahu wa Ta'ala): “Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine” (2: 184).

 Inapendeza kufanya haraka kulipa funga ya Ramadhani lakini mtu akichelewa na kuzilipa kabla ya Ramadhani nyengine kuingia hapana neno. Hii ni kwa mujibu wa kauli ya ‘Aishah (Radhiya Llahu ‘Anha): “Nilikuwa nina deni la Ramadhani, sikuweza kulipa hadi ilipofika mwezi wa Sha‘ban  kwa sababu ya kumhudumikia Mtume wa Allah (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam)” (Al-Bukhaariy na Muslim).

Hivyo, ikiwa Sha‘ban imeingia ni wajibu kwa anayedaiwa funga ya Ramadhani kulipa siku zote kabla Ramadhani mpya kuingia. Mtu akichelewa kulipa siku alizokosa mpaka Ramadhani nyengine kuingia itampasa afunge Ramadhani hii ya sasa na kulipa siku anazodaiwa baada yake. Ikiwa kuchelewa huko kulipa ni kwa sababu ya udhru wa kisheria kama alivyo dada yetu muulizaji swali, kwake itakuwa ni kulipa hiyo miezi miwili peke yake punde tu udhru wa mimba utakapoondoka. 

Na ikiwa mtu hakulipa deni pasi na udhru wowote wa kisheria anawajibika kulipa siku alizokosa za Ramadhani zilizopita pamoja na kulisha masikini kwa kila siku aliyokosa (yaani nusu swaa‘ kama kilo moja na robo).

Bonyeza hapa upate majibu ya maswali yanayohusu kulipa Swawm na fidya:

Kulipa Swawm Na Kafara

 

Na Allah Anajua zaidi