Kufunga Swawm Za Sunnah Siku Tashriyq Haifai
SWALI:
je haifai kufunga yaumul baidh katika mwezi wa dul-hijja na kadhalika sunna ya ijumatatuna alhamisi kwa sababu nilivyo soma katika nasiha za ijumaa, nimefaham ni kwa ajili ya mahujaji tu sio kwa watu waliokua katika mchi zao.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Kufunga masiku hayo ya Ayaamul Biydh (terehe 13, 14, 15 za Kalenda Ya Kiislamu)haitowezekana kwani siku ya kwanza ya Ayaamul-Biydh inaanza tarehe 13 Dhul-Hijjah ambayo ni miongoni mwa siku za Ayaamut-Tashriyq (tarehe 11, 12, 13 Dhul-Hijjah). Inakatazwa kufunga kwa sababu hizi ni siku za kusherehekea kwa kula na kunywa. Na kutokufunga huko ni kwa walio katika Hajj na wasio vilevile.'' Na dalili ni kutokana na Hadiyth ifuatayo:
عن أبي هريرة أن رسول الله صلى الله عليه وسلم بعث عبد الله بن حُذافة يطوف في منى: ((لا تصوموا هذه الأيام، فإنها أيام أكل وشرب، وذكر الله، عز وجل))
Imetoka kwa Abu Hurayrah kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimtuma 'Abdullah bin Hudhaafah azunguke Mina na atangaze "Msifunge siku hizi, kwani hizi ni siku za kula na kunywa na kumkumbuka Allah Mwenye Nguvu Mtukufu' [At-Twabariy:4:211]
Na hizo ndizo siku zilizotajwa kwa ajili ya kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kama Anavyosema katika Aayah ifuatayo:
((وَاذْكُرُواْ اللّهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ))
((Na mtajeni Allah katika zile siku zinazohisabiwa)) [Al-Baqarah:203]
Kwa hiyo haifai kufunga katika siku hizi hata kama mtu alikuwa na mazoea ya kufunga Sunnah za Jumatatu na Alkhamiys au Ayyaamul-Baydh.
Na Allah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
