Kitendo Cha Ndoa Wakati Wa Ramadhaan
SWALI:
Asalam Aleykum! Ndugu zetu waislamu, Mwenyezimungu awajaze na awape subra na muendele kutusaidia na maswali yetu. Inshallah.
Swali langu ni inafaa au ina kubalika kufanya mapenzi au kuingiliana wakati wa ramadhani? Na baada ya kitendo hicho wakaoga na kujitoharisha na kabla ya siku nyengine yaani ya kufunga tena. Na je ikiwa haikubaliki au haifai wafanye nini? na walifanya hivyo
Tafadhali ningependa munijibu maswali yangu
ASANTENI
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allah Mtukufu, Swalah na salamu zimfikie kipenzi chetu, Mtume Muhammad (s.a.w.w.), Ahli zake na Maswahaba zake (r.a.) na Watangu Wema na waliowafuata kwa kheri mpaka Siku ya Kiyama.
Shukrani kwa maswali yako, na hapa tunakupatia majibu yako.
1. Dini ya Kiislamu ambayo ndiyo inakwenda sambamba na maumbile ya mwanadamu inatupatia mwongozo wa kila kitu hata maingiliano baina ya mume na mke, ikiwa ni wakati wa Ramadhaan au baada ya yake. Lakini katika wakati wa Ramadhaan kuna mambo fulani hayafai kufanywa wakati wa mchana japokuwa ni halali kufanywa katika miezi mingine. Na moja katika hayo ni kukutana kimwili baina ya mume na mke wakati wa mchana, lakini baada ya muadhini wa Magharibi wanaweza kufanya mapenzi
Ikiwa mapenzi hayo yalifanywa wakati wa mchana itabidi mume na mke watoe kafara ikiwa wamefanya kitendo hicho kwa makusudi pasina kulazimishwa. Kafara ni ima kuacha mtumwa huru, au kufunga miezi miwili mfululizo au kulisha masikini sitini (Imepokewa na al-Bukhariy na Muslim kutoka kwa Abu Hurayrah [r.a]).
Na kwa maelezo zaidi ingia katika "Fataawa za Ramadhaan" Kuhusu Kulipa Swawm ambazo ziko katika Alhidaaya. Kwa wepesi bonyeza kiungo kifuatacho:
Na Allah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


