Kutokufanya Tendo La Ndoa Kwa Muda Mrefu Kunaleta Madhara?

SWALI:

Assalam alaykum warahmatullah wabarakatuh,

Nawashukuru kwa website yenu kwani anatuelisha sana hasa kwa yale tusiyoyajua,Inshallah Allah awazidishie kila lenye kheri,dunia na akhera.
Swali.Mimi nimsichana wa umri wa miaka 23 na mpaka hivi sasa sijawahi kufanya tendo la ndoa, kwa sasa nimebahatika kupata mchumba lkn kwakweli namshukuru Allah kwani hajawahi hata kunitamkia jambo hilo na nimekuwa na ye
kwa muda mrefu,je ikiwa hujafanya tendo hilo kwa muda mrefu huleta madhara?kwani nimepata tetesi kuwa ikiwa hujafanya jambo hilo kwa muda huleta madhara ya kisaikolojia.

Nitashukuru nikipata ufumbuzi wenye uhakika juu ya jambo hili kwani nashindwa kwa kuwa si jambo jema mbele ya Allah.

Wabillah tawfiq



JIBU:

AlhamduliLLah,  Waswalaatu Was-salaam 'alaa Rasuli-Llah  صلى الله عليه وآله وسلم Amma ba'ad,

Kwanza kabisa inapasa kutambua kuwa sheria ya Kiislamu haimruhusu mtu kuwa na mchumba (boyfriend/girlfriend).  Kufanya hivyo ni kinyume na sheria na katika  kuigiza makafiri.  Na Allaah سبحانه وتعالى   Ametuonya jambo hili kama Anavyosema:

}}وَلَن تَرْضَى عَنكَ الْيَهُودُ وَلاَ النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ{{

 ((Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao))

[Al-Baqarah : 120]

Allaah سبحانه وتعالى Ametuhimiza kuingia katika ndoa kama ilivyo katika Qur'aan:


 ((وَأَنكِحُوا الأََيَامَى مِنكُمْ وَالصَّالِحِينَ مِنْ عِبَادِكُمْ وَإِمَائِكُمْ إِن يَكُونُوا فُقَرَاء يُغْنِهِمُ اللَّهُ مِن فَضْلِهِ وَاللَّهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ))

((Na waozeni wajane miongoni mwenu na wema katika watumwa wenu na wajakazi wenu. Wakiwa mafakiri Mwenyezi Mungu Atawatajirisha kwa fadhila yake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa Mwenye kujua))

An-Nuur:32

Vile vile Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema kuwa kufunga ndoa ni kukamilisha nusu ya dini yake Muislamu kama ilivyo katika Hadiyth ifuatayo       

 روى أنس بن مالك رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وأله وسلم قال ((إذا تزوج العبد ، فقد اسـتكمل نصف الدين فليتق الله فيما بقي )) رواه الطبراني وحسنه الألبان

Imetoka kwa Anas bin Maalik رضي الله عنه  kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema: ((Atakapofunga ndoa mja, huwa amekamilisha nusu ya dini, basi amche Mwenyeezi Mungu kwa nusu iliyobaki )) 

[At-Twabaraaniy, na Sheikh Albaaniy amesema ni Hasan]

Muislamu anatakiwa kutimiza Sunnah hii ya kufunga ndoa bila ya kuchelewa kuepukana na madhara mingi. Kwa hiyo ndugu yetu tunakupa nasaha muhimu yenye manufaa kuwa ingia katika ndoa na huyo mchumba madam ni Muislamu na hatuoni   kuwa umetaja sababu yoyote ya kukuzuia kufunga naye ndoa.  

Na ikiwa hukuweza kufunga ndoa kwa muda wowote kwa sababu fulani  basi inakupasa ujihifadhi na kujiweka katika heshima na stara hadi utakapojaaliwa kufunga ndoa kama Alivyotuamrisha Allaah سبحانه وتعالى  

((وَلْيَسْتَعْفِفِ الَّذِينَ لَا يَجِدُونَ نِكَاحًا حَتَّى يُغْنِيَهُمْ اللَّهُ مِن فَضْلِهِ ..  ))

((Na wajizuilie na machafu wale wasiopata cha kuolea, mpaka Mwenyezi Mungu Awatajirishe kwa fadhila yake))

[An-Nuur:  33]

Kuchelewa kuolewa haina maana kwamba itakuletea madhara ya kisaikolojia ikiwa utabakia katika Twa'a ya Allaah سبحانه وتعالى , kwani hayo ni katika majaaliwa ya Allaah سبحانه وتعالى  na muumini anatakiwa akubali na kuridhika majaaliwa yote. Bali huenda ikaleta madhara hayo ikiwa utakuwa mbali na Twa'a.


Na hizi habari za kupata madhara ya kisaikolojia, zimeletwa na Makafiri wanaotaka kuwatoa waislam katika maadili yao kwa kuwahamasisha kufanya uzinifu. Na hasa ziko sana fikra hizo katika nchi za nje kama Ulaya na Marekani ambako uzinzi ni sehemu ya maisha.  Watoto tangu shule wanakuwa na marafiki wa jinsia tofauti na kuanza kufanya uzinifu bado wakiwa wadogo hata wengine wanaanza kujaribu wakiwa hawajabaleghe bado! Kwa hali hiyo, wanaamini kuwa kama mtu hana rafiki na hafanyi tendo la ndoa, basi lazima ana matatizo na huenda hata akachanganyikiwa baadaye!! 

Na ndio maana  Mtume صلى الله عليه وآله وسلم aliamrisha kuwa ni bora kufunga kwa yule ambaye hakuweza kufunga ndoa ili kuepukana na hatari ya maasi kama kuingia katika zinaa.

))يَا مَعْشَرَ الشَّبَابِ مَنْ اسْتَطَاعَ الْبَاءَةَ فَلْيَتَزَوَّجْ فَإِنَّهُ أَغَضُّ لِلْبَصَرِ وَأَحْصَنُ لِلْفَرْجِ وَمَنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَعَلَيْهِ بِالصَّوْمِ فَإِنَّهُ لَهُ وِجَاءٌ((  البخاري   ومسلم

((Enyi vijana, anayeweza kuoa   basi na aowe  kwani ni lindo la macho (na kutazama ya kutamanisha) na ni hifadhi ya tupu (kwa kufanya zinaa) Na asiyeweza basi afunge (Swawm) kwani ni kinga (ya matamanio) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 Wa Allaahu A'alam.

 

Share