001 - Swali La 1: Ni jambo Gani La Mwanzo Linalopasa Waja

Swali La 1:

 

ما أول ما يجب على العباد؟

Ni jambo gani la mwanzo linalopasa waja?

 

Jibu: 

 

أول ما يجب على العباد معرفة الأمر الذي خلقهم الله له, وأخذ عليهم الميثاق به وأرسل به رسله إليهم وأنزل به كتبه عليهم, ولأجله خلقت الدنيا والآخرة والجنة والنار وبه حقت الحاقة ووقعت والواقعة وفي شأنه تنصب الموازين وتتطاير الصحف وفيه تكون الشقاوة والسعادة وعلى حسبه تقسم الأنوار

La mwanzo linalopasa kwa waja ni: Kujua kusudio la Allaah (سبحانه وتعالى) la kuwaumba wao. Kuchukua ahadi nzito kutoka kwao, kuwatumia Mitume, kuwashushia kwayo vitabu Vyake. Na kwa ajili yake dunia na Aakhirah imeumbwa, na Pepo na Moto,  na imehakiki la kuhakiki na litatokea la kutokea na jambo hilo Mizani zitawekwa, na Swahifa zitatawanywa, na kutakuwa na huzuni na furaha, na kwa mnasaba huo kutagawanywa Nuru.

 

وَمَن لَّمْ يَجْعَلِ اللَّـهُ لَهُ نُورًا فَمَا لَهُ مِن نُّورٍ

Na ambaye Allaah Hakumjaalia Nuru, basi hawi na Nuru.[1]

 

 

 

 

 

 [1] An-Nuwr (24: 40).

 

Share