Sha'baan: Tanabahi Bid'ah Ya Nusu Ya Sha’baan; Swawm, Dhikru-Allaah, Kuomba Du’aa

 

Tanabahi Kuhusu Bid'ah Za Niswfu Sha’baan; Swawm, Adkhaar Na Kuomba Du’aa

 

 Alhidaaya.com

 

 

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi waa alihi wa sallam) ametahadharisha kuhusu bid’ah aliposema:

 

 ((أُوصِيكُمْ بِتَقْوى اللَّه، وَالسَّمْعِ وَالطَّاعَةِ وإِنْ تَأَمَّر عَلَيْكُمْ عَبْدٌ حبشيٌ، وَأَنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ فَسَيرى اخْتِلافاً كثِيرا. فَعَلَيْكُمْ بسُنَّتي وَسُنَّةِ الْخُلُفَاءِ الرَّاشِدِينَ الْمَهْدِيِّينَ، عضُّوا عَلَيْهَا بالنَّواجِذِ، وإِيَّاكُمْ ومُحْدثَاتِ الأُمُورِ فَإِنَّ كُلَ بِدْعَةٍ ضلالَةٌ)) رواه أبو داود، والترمذِي وقال حديث حسن صحيح

((Nakuusieni kumcha Allaah, usikivu na twaa hata ikiwa kiongozi wenu (Au atakayekuamrishen) ni Mtumwa wa Habash. Mtakaoishi miongoni mwenu mtaona ikhtilafu nyingi. Kwa hiyo shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Makhalifa waliongoka baada yangu.  Ziumeni kwa magego (zikamateni kwa nguvu wala msiziache). Na tahadharini na mambo ya uzushi kwani kila bid'ah ni upotofu)) [Abu Daawuwd, At-Trimidhiy kasema Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Na katika Riwaayah nyingine alikuwa kila alipokhutubia akitanguliza kusema:

 

أَمَّا بَعْدُ ،  فَإِنَّ خَيْرَ اَلْحَدِيثِ كِتَابُ اَللَّهِ ، وَخَيْرَ اَلْهَدْيِ هَدْي ُ‏ مُحَمَّدٍ ، وَشَرَّ اَلْأُمُورِ مُحْدَثَاتُهَا، وَكُلَّ بِدْعَةٍ ضَلَالَة  ،رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Ammaa Ba’du, Hakika Maneno bora kabisa ni  Kitabu cha Allaah (Qur-aan) na mwongozo bora kabisa ni mwongozo wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), na uovu zaidi wa mambo ni yale yenye kuzushwa (bila dalili ya kisharia), na kila bid'ah ni upotofu. [Muslim]

 

 

Swali:

 

“Je, bid’ah, hata bid’ah hiyo iwe ndogo vipi ni miongoni mwa madhambi makubwa? Au kuna ufafanuzi bayana wa hili?”

 

Jibu:

 

“Swali hilo jibu lake ni fupi! Swali hilo si sahihi (halikubaliki kuulizwa)! Na wala haliko katika manhaj ya Salaf. Kuweka vigawanyo, na kupiga mifano na mabishano ya kukubali bid’ah kwa kuhusisha na  dhambi si katika manhaj ya Salaf!

 

Salaf walikuwa wakipinga bid’ah kikamilifu bila ya kuwekea mipaka kama walivyokuwa wakipinga dhambi, huku wakichukulia jambo la (bid’ah) kuwa ni dhambi. Lakini walilolitilia nguvu kulikataza lilikuwa ni bid’ah na hivyo lilikuwa kwao ni jambo kuu!

 

Na vyovyote tutakavyotaka kuingia katika maudhui ya bid’ah na kutaka kuigawa katika bid’ah kubwa na ndogo, au aina za bid’ah (hoja inayotolewa kuunga mkono bid’ah kwamba ni: “bid’atun hasanah”), na mengineyo, basi mtu huyo hana isipokuwa analotaka ni kuwafanyia watu njia walichukulie jambo la bid’ah kuwa ni jambo jepesi. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikariri (katika khutbah zake):  

 

 وكل بدعة ضلالة وكل ضلالة في النار 

Na kila bid'ah ni upotofu, na kila upotofu ni motoni.  

 

 

Kwa hiyo tunamwambia muulizaji kwamba: “Baina yako na sisi ni Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

وكل بدعة ضلالة وكل ضلالة في النار 

Na kila bid'ah ni upotofu, na kila upotofu ni motoni.  

 

 

Na huenda mmoja wenu akasema: “Vizuri! Lakini huenda ikawa ipo (bid’ah) ndogo”.  Basi namjibu: “Njoo hapa! Njoo hapa usikilize Hadiyth za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na simulizi za Salaf.

 

Ama katika Hadiyth ni wale watu watu ambao mmoja wao alisema: “Mimi nitaswali usiku wote.” Mwengine akasema: “Mimi nitafunga mchana na wala sitofungulia swawm.” Na wa tatu akasema: “Mimi nitajiweka mbali na wanawake na sitooa.”

 

Hao watu watatu walitaka kutekeleza vitendo hivyo wakidhania kwamba wanajikurubisha kwa Allaah (‘Azza wa Jalla). Lakini je, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaambia nini? Je aliwaambia: “Hayo ni mambo mepesi na sahali lakini yaacheni na Allaah Akujazeni khayr?” 

 

Hapana! Bali aliwajibu:

 

Ama mimi ninafunga na kufungua, ninaswali na kulala, ninaoa wanawake. Kwa hivyo yeyote anayegeuka kinyume na Sunnah yangu si miongoni mwangu!

 

Tazama aliwajibu nini! Aliwajibu:

 

Yeyote anayegeuka kinyume na Sunnah (uongofu) yangu sio miongoni mwangu!.

 

Huo ni mfano mmoja wa Hadiyth.  Ama katika simulizi za Swahaabah, ni usimulizi wa Ibn Mas‘uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuhusu watu walioketi kwa mzunguko wa duara Msikitini. Je walikuwa wakifanya nini?

 

Walikuwa wakimsabbih Allaah (wakisema: Subhaanah Allaah), wakimsifu Allaah (wakisema: AlhamduliLLaah), wakimpwekesha Allaah (wakisema: Laa ilaaha illa Allaah), wakimtukuza Allaah (wakisema: Allaahu Akbar). [Usimulizi kamili wa tukio hilo upo chini].

 

Je, walikuwa wako wapi watu hao? Je walikuwa disco? Au katika kiwanja cha michezo? Au katika baa? Hapana! Walikuwa wako Msikitini! Je, Ibn Mas-‘uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) aliwaambia nini? Aliwaambia:  

 

"Naapa kwa Yule Ambaye roho yangu ipo mikononi Mwake! Aidha mupo kwenye njia (Dini) iliyoongoka zaidi kuliko njia ya Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ama munafungua milango ya upotofu!”

 

Hakuwaambia: “Naapa kwa Allaah, vitendo vyenu si sahihi lakini ni bid’ah ndogo Allaah Awahidi! Na bid’ah ndogo dhambi yake ni ndogo kuliko bid’ah kubwa, kwa hiyo acheni jambo hili Allaah Awabariki! Na watu watendao bid’ah kubwa dhambi zao ni kubwa kuliko nyinyi mnaofanya bid’ah ndogo!”

 

Hapana! Hapana! Hapana!   

 

Bali aliwaambia: “Aidha mpo kwenye dini iliyoongoka zaidi kuliko Dini ya Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ama mnafungua milango ya upotofu!”

 

Hakuna kuyumbayumba wala kulifunika jambo, bali ni kudhihirisha haki au ubatilifu. Inapohusu Sunnah na bid’ah, basi ima ni haki au ubatilifu! Ndio maana maneno haya yatiliwe manani kama nilivyotaja awali.

 

[Usimulizi uliotimia wa kadhia hiyo ya watu waliokuwa wamekusanyika kumdhukuru Allaah Msikitini]:

 

عن عمرو بن سلمة (رضي الله عنه): كُنَّا نَجْلِسُ عَلَى بَابِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ قَبْلَ صَلاَةِ الْغَدَاةِ فَإِذَا خَرَجَ مَشَيْنَا مَعَهُ إِلَى الْمَسْجِدِ, فَجَاءَنَا أَبُو مُوسَى الأَشْعَرِيُّ فَقَالَ: َخَرَجَ إِلَيْكُمْ أَبُو عَبْدِ الرَّحْمَنِ بَعْدُ؟ قُلْنَا لاَ:  فَجَلَسَ مَعَنَا حَتَّى خَرَجَ, فَلَمَّا خَرَجَ قُمْنَا إِلَيْهِ جَمِيعًا فَقَالَ لَهُ أَبُو مُوسَى: يَا أَبَا عَبْدِ الرَّحْمَنِ إِنِّي رَأَيْتُ فِي الْمَسْجِدِ آنِفًا أَمْرًا أَنْكَرْتُهُ وَلَمْ أَرَ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ إلاَّ خَيْرًا. قَالَ: فَمَا هُوَ؟ فَقَالَ: إِنْ عِشْتَ فَسَتَرَاهُ. قَالَ: رَأَيْتُ فِي الْمَسْجِدِ قَوْمًا حِلَقًا جُلُوسًا يَنْتَظِرُونَ الصَّلاَةَ, فِي كُلِّ حَلْقَةٍ رَجُلٌ وَفِي أَيْدِيهِمْ حَصًى. فَيَقُولُ, كَبِّرُوا مِائَةً ,فَيُكَبِّرُونَ مِائَةً, فَيَقُولُ هَلِّلُوا مِائَةً, فَيُهَلِّلُونَ مِائَةً, وَيَقُولُ سَبِّحُوا مِائَةً, فَيُسَبِّحُونَ مِائَةً, قَالَ: فَمَاذَا قُلْتَ لَهُمْ ؟ قَالَ:  مَا قُلْتُ لَهُمْ شَيْئًا انْتِظَارَ رَأْيِكَ وَانْتِظَارَ أَمْرِكَ. قَالَ أَفَلاَ أَمَرْتَهُمْ أَنْ يَعُدُّوا سَيِّئَاتِهِمْ وَضَمِنْتَ لَهُمْ أَنْ لاَ يَضِيعَ مِنْ حَسَنَاتِهِمْ؟  ثُمَّ مَضَى وَمَضَيْنَا مَعَهُ حَتَّى أَتَى حَلْقَةً مِنْ تِلْكَ الْحِلَقِ فَوَقَفَ عَلَيْهِمْ فَقَالَ. مَا هَذَا الَّذِي أَرَاكُمْ تَصْنَعُونَ؟ قَالُوا: يَا أَبَا عَبْدِ الرَّحْمَنِ حَصًى نَعُدُّ بِهِ التَّكْبِيرَ وَالتَّهْلِيلَ وَالتَّسْبِيحَ. قَالَ: فَعُدُّوا سَيِّئَاتِكُمْ فَأَنَا ضَامِنٌ أَنْ لاَ يَضِيعَ مِنْ حَسَنَاتِكُمْ شَيْءٌ وَيْحَكُمْ يَا أُمَّةَ مُحَمَّدٍ, مَا أَسْرَعَ هَلَكَتَكُمْ هَؤُلاَءِ صَحَابَةُ نَبِيِّكُمْ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) مُتَوَافِرُونَ وَهَذِهِ ثِيَابُهُ لَمْ تَبْلَ وَآنِيَتُهُ لَمْ تُكْسَرْ. وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ إِنَّكُمْ لَعَلَى مِلَّةٍ هِيَ أَهْدَى مِنْ مِلَّةِ مُحَمَّدٍ أَوْ مُفْتَتِحُو بَابِ ضَلاَلَةٍ. قَالُوا: وَاللَّهِ يَا أَبَا عَبْدِ الرَّحْمَنِ مَا أَرَدْنَا إِلاَّ الْخَيْرَ. قَالَ وَكَمْ مِنْ مُرِيدٍ لِلْخَيْرِ لَنْ يُصِيبَهُ.  إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) حَدَّثَنَا أَنَّ قَوْمًا يَقْرَءُونَ الْقُرْآنَ لاَ يُجَاوِزُ تَرَاقِيَهُمْ وَايْمُ اللَّهِ مَا أَدْرِي لَعَلَّ أَكْثَرَهُمْ مِنْكُمْ.  ثُمَّ تَوَلَّى عَنْهُمْ فَقَالَ عَمْرُو بْنُ سَلَمَةَ: رَأَيْنَا عَامَّةَ أُولَئِكَ الْحِلَقِ يُطَاعِنُونَا يَوْمَ النَّهْرَوَانِ مَعَ الْخَوَارِجِ.

Kutoka kwa ‘Amru bin Salamah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Tulikuwa tumeketi mlangoni mwa ‘Abdullaah bin Mas’uwd kabla ya Swalaah ya Alfajiri, akatoka nje. Tukaenda naye Msikitini. Kisha Abuu Muwsaa Al-Ash’ariyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akatujia na kusema: “Je, Abuu ‘Abdir-Rahmaan ameshakuja kwenu?” Tukasema: “Hapana!” Akaketi hadi akatoka nje na alipotoka nje tukasimama. Abuu Muwsaa akamwambia: “Ee Abaa ‘Abdir-Rahmaan! Sasa hivi nimeona jambo Msikitini sijapatapo kuliona kabla, lakini sidhanii baya ila ni jambo jema”. Akasema: “Jambo gani?” Akasema. “Ukiendelea kuishi utaliona”. Akasema: “Nimeona Msikitini watu wameketi kwa mkusanyiko wa duara wakisubiri Swalaah. Katika kila duara alikuweko mtu na mikononi mwao mna changarawe. Mmoja wao akisema: “Semeni Allaahu Akbar mara mia!” nao wakisema “Allaahu Akbar!” mara mia. Kisha husema: “Semeni laa ilaaha illa-Allaah mara mia”! Nao husema “laa ilaaha illa-Allaah!” mara mia. Kisha husema: “Semeni Subhaana-Allaah mara mia!” Nao husema “Subhaana-Allaah!” mara mia. Akasema: “Je umewaambia nini?” Nikasema: “Sikusema lolote, nilikuwa nasubiri nione utaonaje na nikisubiri amri yako”. Akasema: “Kwa nini usiwaambie wahesabu vitendo vyao viovu na kuwahakikishia kwamba vitendo vyao vyema havitopotezwa?”

 

Kisha akasogea nasi tukaenda hadi alipofikia moja kati ya maduara hayo akasimama na kusema: “Mnafanya nini?” Wakasema. “Ee Abaa ‘Abdir-Rahmaan, hivi ni vijiwe tunavyohesabia takbiyr, tahliyl na tasbiyh”. Akasema: “Hesabuni vitendo vyenu viovu, kwani nakuhakikisheni kwamba vitendo vyenu vyema havitopotea hata kimoja! Ole wenu Ee Ummah wa Muhammad! Ni kwa haraka gani mnakimbilia kwenye uharibifu! Hawa ni Maswahaba wa Nabiy wenu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambao wameenea. Hizi ndizo nguo zake ambazo bado hazijachakaa, na bakuli lake ambalo halijavunjika! Naapa kwa Yule Ambaye roho yangu ipo mikononi Mwake! Aidha mpo kwenye dini iliyoongoka zaidi kuliko Dini ya Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ama mnafungua milango ya upotofu!”

 

Wakasema: “Ee Abaa ‘Abdir-Rahmaan, hatukukusudia lolote ila khayr tu”. Akasema: “Wangapi waliokusudia khayr hawakuzipata?” Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuambia: ((Watu wataisoma Qur-aan, lakini haitovuka zaidi ya koo zao)) “Naapa kwa Allaah! Mimi sijui, lakini pengine mengi kati ya hayo yanatoka kwenu!” Baadaye akaondoka. ‘Amr bin Salamah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Tumewaona wengi kati ya watu hao wakipigana dhidi yetu katika siku ya Nahrawaan, wakiwa pamoja na Khawaarij [Sunan Ad-Darimy 206 – Ameisahihisha Al-Albaaniy katika As-Silsilah Asw-Swahiyhah (5/11)]

 

 

 

 

Share