055 - Ar-Rahmaan
الرَّحْمن
Ar-Rahmaan: 055
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الرَّحْمَـٰنُ ﴿١﴾
1. Ar-Rahmaan.
عَلَّمَ الْقُرْآنَ ﴿٢﴾
2. Amefundisha Qur-aan.
خَلَقَ الْإِنسَانَ ﴿٣﴾
3. Ameumba binaadamu.
عَلَّمَهُ الْبَيَانَ ﴿٤﴾
4. Amemfunza ufasaha.
الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ بِحُسْبَانٍ ﴿٥﴾
5. Jua na mwezi huenda katika hesabu.
وَالنَّجْمُ وَالشَّجَرُ يَسْجُدَانِ ﴿٦﴾
6. Na nyota na miti vinasujudu.
وَالسَّمَاءَ رَفَعَهَا وَوَضَعَ الْمِيزَانَ ﴿٧﴾
7. Na mbingu Ameziinua na Akaweka mizani.
أَلَّا تَطْغَوْا فِي الْمِيزَانِ ﴿٨﴾
8. Ili msivuke mipaka (kudhulumu) katika mizani.
وَأَقِيمُوا الْوَزْنَ بِالْقِسْطِ وَلَا تُخْسِرُوا الْمِيزَانَ ﴿٩﴾
9. Na simamisheni uzani kwa uadilifu, na wala msipunguze mizani.
وَالْأَرْضَ وَضَعَهَا لِلْأَنَامِ ﴿١٠﴾
10. Na ardhi Ameiweka chini kwa ajili ya viumbe.
فِيهَا فَاكِهَةٌ وَالنَّخْلُ ذَاتُ الْأَكْمَامِ ﴿١١﴾
11. Humo mna matunda na mitende yenye mafumba.
وَالْحَبُّ ذُو الْعَصْفِ وَالرَّيْحَانُ ﴿١٢﴾
12. Na nafaka zenye makapi na rehani; miti yenye harufu nzuri ya kunukia.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿١٣﴾
13. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
خَلَقَ الْإِنسَانَ مِن صَلْصَالٍ كَالْفَخَّارِ ﴿١٤﴾
14. Amemuumba binaadamu kutokana na udongo wa mfinyanzi unaotoa sauti kama udongo wa kinamo.
وَخَلَقَ الْجَانَّ مِن مَّارِجٍ مِّن نَّارٍ ﴿١٥﴾
15. Na Akaumba majini kutokana na mwako wa moto.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿١٦﴾
16. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
رَبُّ الْمَشْرِقَيْنِ وَرَبُّ الْمَغْرِبَيْنِ ﴿١٧﴾
17. Rabb wa Mashariki mbili na Rabb wa Magharibi mbili.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿١٨﴾
18. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
مَرَجَ الْبَحْرَيْنِ يَلْتَقِيَانِ ﴿١٩﴾
19. Ameziachilia bahari mbili zinakutana.
بَيْنَهُمَا بَرْزَخٌ لَّا يَبْغِيَانِ ﴿٢٠﴾
20. Baina yake kuna kizuizi, hazivukiani mipaka.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٢١﴾
21. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
يَخْرُجُ مِنْهُمَا اللُّؤْلُؤُ وَالْمَرْجَانُ ﴿٢٢﴾
22. Zinatoka humo lulu na marijani.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٢٣﴾
23. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
وَلَهُ الْجَوَارِ الْمُنشَآتُ فِي الْبَحْرِ كَالْأَعْلَامِ ﴿٢٤﴾
24. Na ni Vyake vyombo viendavyo baharini vikiinuliwa tanga kama milima.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٢٥﴾
25. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ ﴿٢٦﴾
26. Kila aliyekuwa juu yake (ardhi) ni mwenye kutoweka.
وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ ﴿٢٧﴾
27. Na utabakia Wajihi wa Rabb wako Mwenye Ujalali na Ukarimu.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٢٨﴾
28. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
يَسْأَلُهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ كُلَّ يَوْمٍ هُوَ فِي شَأْنٍ ﴿٢٩﴾
29. Wanamuomba Yeye wote walio mbinguni na ardhini, kila siku Yeye Yumo katika Kubadilisha mambo.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٣٠﴾
30. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
سَنَفْرُغُ لَكُمْ أَيُّهَ الثَّقَلَانِ ﴿٣١﴾
31. Tutakukusudieni kwa hisabu enyi aina mbili ya viumbe; majini na wanaadamu.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٣٢﴾
32. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ إِنِ اسْتَطَعْتُمْ أَن تَنفُذُوا مِنْ أَقْطَارِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ فَانفُذُوا ۚ لَا تَنفُذُونَ إِلَّا بِسُلْطَانٍ ﴿٣٣﴾
33. Enyi jamii ya majini na wanaadamu! Mkiweza kupenya kwenye zoni za mbingu na ardhi, basi penyeni. Hamtoweza kupenya isipokuwa kwa mamlaka (ya Allaah).
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٣٤﴾
34. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
يُرْسَلُ عَلَيْكُمَا شُوَاظٌ مِّن نَّارٍ وَنُحَاسٌ فَلَا تَنتَصِرَانِ ﴿٣٥﴾
35. Mtapelekewa mwako wa moto juu yenu na shaba iliyoyayushwa, basi hamtoweza kujinusuru.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٣٦﴾
36. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
فَإِذَا انشَقَّتِ السَّمَاءُ فَكَانَتْ وَرْدَةً كَالدِّهَانِ ﴿٣٧﴾
37. Zitakapoachana mbingu zikawa rangi ya waridi kama mafuta.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٣٨﴾
38. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُسْأَلُ عَن ذَنبِهِ إِنسٌ وَلَا جَانٌّ ﴿٣٩﴾
39. Siku hiyo hatoulizwa kuhusu dhambi yake binaadamu wala jini.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٤٠﴾
40. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
يُعْرَفُ الْمُجْرِمُونَ بِسِيمَاهُمْ فَيُؤْخَذُ بِالنَّوَاصِي وَالْأَقْدَامِ ﴿٤١﴾
41. Watatambulikana wahalifu kwa alama zao, basi watachukuliwa kwa vipaji vya uso na miguu.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٤٢﴾
42. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
هَـٰذِهِ جَهَنَّمُ الَّتِي يُكَذِّبُ بِهَا الْمُجْرِمُونَ ﴿٤٣﴾
43. Hii ni Jahannam ambayo wahalifu wanaikadhibisha.
يَطُوفُونَ بَيْنَهَا وَبَيْنَ حَمِيمٍ آنٍ ﴿٤٤﴾
44. Wataizunguka baina yake na baina ya maji yachemkayo yaliyofikia ukomo wa kutokota.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٤٥﴾
45. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
وَلِمَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ جَنَّتَانِ ﴿٤٦﴾
46. Na kwa mwenye kukhofu kisimamo mbele ya Rabb wake atapata bustani mbili.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٤٧﴾
47. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
ذَوَاتَا أَفْنَانٍ ﴿٤٨﴾
48. Zilizo na matawi yaliyotanda.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٤٩﴾
49. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
فِيهِمَا عَيْنَانِ تَجْرِيَانِ ﴿٥٠﴾
50. Mna humo chemchemu mbili zinazopita.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٥١﴾
51. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
فِيهِمَا مِن كُلِّ فَاكِهَةٍ زَوْجَانِ ﴿٥٢﴾
52. Mna humo kila matunda ya aina mbilimbili.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٥٣﴾
53. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
مُتَّكِئِينَ عَلَىٰ فُرُشٍ بَطَائِنُهَا مِنْ إِسْتَبْرَقٍ ۚ وَجَنَى الْجَنَّتَيْنِ دَانٍ ﴿٥٤﴾
54. Wakiegemea kwenye matandiko ya kupumzikia, bitana yake ni kutokana na hariri nzito nyororo, na matunda ya bustani mbili yako karibu na kufikiwa.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٥٥﴾
55. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
فِيهِنَّ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَانٌّ ﴿٥٦﴾
56. Mna humo wanawake wenye staha wanaoinamisha macho, hajawabikiri kabla yao binaadamu yeyote wala jini.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٥٧﴾
57. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
كَأَنَّهُنَّ الْيَاقُوتُ وَالْمَرْجَانُ ﴿٥٨﴾
58. Kama kwamba hao wanawake ni yakuti na marijani.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٥٩﴾
59. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
هَلْ جَزَاءُ الْإِحْسَانِ إِلَّا الْإِحْسَانُ ﴿٦٠﴾
60. Je, kuna jazaa ya ihsani isipokuwa ihsani tu?
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٦١﴾
61. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
وَمِن دُونِهِمَا جَنَّتَانِ ﴿٦٢﴾
62. Na zaidi ya hizo mbili, ziko bustani mbili zingine.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٦٣﴾
63. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
مُدْهَامَّتَانِ ﴿٦٤﴾
64. Za rangi ya kijani iliyokoza.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٦٥﴾
65. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
فِيهِمَا عَيْنَانِ نَضَّاخَتَانِ ﴿٦٦﴾
66. Mna humo chemchemu mbili zenye kububujika kwa nguvu mfululizo.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٦٧﴾
67. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
فِيهِمَا فَاكِهَةٌ وَنَخْلٌ وَرُمَّانٌ ﴿٦٨﴾
68. Mna humo matunda na mitende na makomamanga.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٦٩﴾
69. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
فِيهِنَّ خَيْرَاتٌ حِسَانٌ ﴿٧٠﴾
70. Mna humo wanawake wazuri, wema.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٧١﴾
71. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
حُورٌ مَّقْصُورَاتٌ فِي الْخِيَامِ ﴿٧٢﴾
72. Hurulaini: Wanawake weupe wazuri wa Jannah wenye macho makubwa ya kupendeza, wanaotawishwa katika mahema.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٧٣﴾
73. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَانٌّ ﴿٧٤﴾
74. Hajawabikiri kabla yao binaadamu yeyote wala jini.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٧٥﴾
75. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
مُتَّكِئِينَ عَلَىٰ رَفْرَفٍ خُضْرٍ وَعَبْقَرِيٍّ حِسَانٍ ﴿٧٦﴾
76. Wakiegemea kwenye matakia ya kijani na mazulia ya rangi mbalimbali ya hariri mazuri mno yasiyo na kifani.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٧٧﴾
77. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
تَبَارَكَ اسْمُ رَبِّكَ ذِي الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ ﴿٧٨﴾
78. Limebarikika Jina la Rabb wako Mwenye Ujalali na Ukarimu.
