Swali La Nyongeza Katika Majibu ya Swali La Mume Wangu Hapendi Kustarehe Na Mimi


SWALI:

assalamu alykum  nimefurahi  sana kwajawabu zenu    tatizo hililimeanza zamani tangu bada ya kuoana ,.
  1) tatizo
hilo  tangu baada ya kuaona 

2) ndio tumepata watoto  lkn kwakudra ya mungu mwen yewe.

3) tumeoana kijamaa 

4) yey mwenyewe ndio alonitaka na mwenyewe nimemkubali.

5) hatukuwahi kupendana kimapenzi wala kukatana kimapenzi.

6) tokea  awali ndio hivi hivi.

7) naishi mm na mume wangu tu

lkn nashukur  mungu katupa watoto pia mume wangu hali miraa wla hatizami  film za ngono pia sikuwahi kumuona na habri hizo za kujichua. na hao wanawake sina uhakika  kama anfanya nao wla vipi  lkn nishawahikuonamsg  number za cmna pia kachat na mwanamke na kumstarehesha kwa maneno   kwa hiyo mm inshAllaah nimo kusubiri nantasubiri lkn nimechoka kifkra sijui kakusudia nini ikiwa mm hawezi kustarehe na mimi lkn huu anpenda wanwake.

 

 


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa dada yetu kwa nyongeza hizo. Lakini ibara nyingine zimekatwa katwa au hazieleweki ili kuweza kutoa nasaha za kina na za kutosheleza.

Hata hivyo, sisi hapa tunasema yafuatayo baada ya maelezo hayo:

 

1.    Ikiwa tatizo hilo lilikuwa kuanzia muoane inaonyesha ana tatizo. Kwa hiyo, ni vyema uzungumze naye mumeo, kijamaa na kama mke wake ili muweze kwenda kuonana na daktari aliyebobea katika magonjwa ya kiume. Kwa kufanya hivyo, inawezekana ikapatikana dawa ya kuweza kumsaidia kuweza kustarehe nawe.

2.  Huenda ikawa amesikia sifa zako au kwa sababu ya ujamaa alipendekewa akuoe kupitia kwa mzazi wake lakini yeye hakuwa na mapenzi nawe. Kwa kuwaridhisha wazazi wake alifanya hivyo ndivyo hahisi kabisa kustarehe nawe.

3.    Inawezekana kuwa kwa kuwasiliana na mwanamke au wanawake wengine akawa anaona aoe mwingine au anaona kwa kufanya hivyo utataka talaka ili isionekane yeye ndio hakutaki. Kwa hiyo, akapata fursa ya kumuoa amtakae kwa ridhaa yake bila kuelekezwa na mtu mwingine.

4.   Tatizo kama hilo huwa bila shaka linashosha kifikra, kiakili, kifiziolojia na ikiwa shida hiyo haitatatuliwa mapema huenda ikakufishika sehemu mbaya sana.

Kwa tatizo lilivyo tunaona unaweza kufanya yafuatayo:

 

1. Ukae na mumeo kama wanandoa na mzungumze kiutu uzima hilo tatizo kwa uwazi na bila kuficha. Ikiwa kila mmoja atakuwa wazi kwa mwenziwe huenda suluhisho ikapatikana kwa usahali kabisa

 

2. Ikiwa hatua hiyo ya kwanza haikuzaa natija yoyote, bila shaka itakuwa muhimu sana kwa wazazi wa kila upande waje katika mkutano wa kutaka upatanishi na tatizo hilo sugu baina yenu. Allaah Aliyetukuka Ameahidi kuwa lau kila upande utakuja katika kikao hicho kwa nia nzuri, ikhlasi na kutaka upatano basi suluhisho la kudumu litapatikana

 

3. Ikiwa hakuna suluhisho lolote basi itabidi mutengane na jambo hilo litakuwa bora kwa kila mmoja. Kufanya hivyo, itampatia fursa kila mmoja kuweza kupata mwendani mwengine ambaye ataweza kuridhiana naye kwa kiasi kikubwa zaidi. Hili litafanyika tu ikiwa njia nyingine hazikufaulu.

Tunakuombea kwa Mola wetu Mlezi Akuwafikie na kukuondolea tatizo hilo kwa wakati muafaka kabisa.

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

Share